Dar es Salaam, Tanzania – Nipe Fagio, taasisi isiyo ya kiserikali inayofanyakazi na jamii, sekta binafsi, na serikali ili kufikia maendeleo endelevu katika sekta ya usimamizi wa taka, imezindua kampeni ijulikanayo kama “Thamini Waokota Taka” yenye lengo la kuubadirisha mtazamo wa jamii dhidi ya waokota taka nchini.
Kampeni ya “Thamini Waokota Taka” imezinduliwa ikiwa kama harakati zinazolenga katika kutambua umuhimu wa waokota taka katika sekta ya usimamizi wa taka na kuhimiza ulazima wa kuwapatia waokota taka mazingira salama ya ufanyaji kazi, jamii kuwatambua, na haki ya kulindwa katika nyakati za majanga kama COVID-19. Kampeni hiyo ikienda pamoja na kampeni ya kidunia ijulikanayo kama “Not Disposable” yaani “Si Yakutupwa” inayoendeshwa na taasisi ya Break Free From Plastic, ambayo pia ni moja ya harakati inayoiangazia dunia ya baadae iliyohuru dhidi ya uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki.
Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio, Bi. Ana Le Rocha, amesema kuwa waokota taka ni wafanyakazi muhimu sana katika sekta ya usimamizi taka na mazingira kwa wanasaidia kuhakikisha kuwa taka rejeshi zinakusanywa, na kuzisimamia vizuri taka ngumu katika jamii zetu.
“Kupitia ukusanyaji wa taka Dar es Salaam nzima, waokota taka husaidia kuongeza kiwanga cha urejeleshaji taka na kupunguza kiwango cha taka au vitu vinavyotupwa katika mazingira yetu. Kazi yao ni lazima ithaminiwe kwa mchango wake wa kufanya tuwe na mazingira safi na makazi yaliyosalama kiafya.
“Nipe Fagio inafanyakazi kwa ukaribu mkubwa sana na waokota taka na tunaamini kuwa, wakiwa kama wafanyakazi muhimu, wanahaki ya kuwa na mazingira salama ya kazi, na wanahitaji kulindwa katika nyakati za majanga kama COVID-19,” alisema Bi. Rocha.
Bi. Rocha aliongeza: “Waokota taka ni wataalamu kwenye hii sekta ya usimamizi taka na wenye uwezekano wa kuendelea kuchangia zaidi kwenye lengo la kuwa na Tanzania safi”.
Manispaa ya jiji la Dar es Salaam inakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 5,600 za taka kwa siku. Chini ya asilimia 40 ya taka hizo zizalishwazo uishia kwenye dampo lililopo. Taka zilizosalia ambazo hazikukusanywa uishia kwenye maeneo ya wazi, mito, barabarani, mifumo ya maji taka na baharini. Waokota taka ni muhimu sana katika kupunguza uwiano huu.
No comments:
Post a Comment