Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakari Kunenge (aliyekunja mikono) na ujumbe wake akiwa ndani ya machinjio ya kisasa Vingunguti. |
Ng’ombe aliyechinjwa kwa ajili ya majaribio akiwa amenyanyuliwa kwa mashine tayari kwa ajili ya kuchunwa ngozi na kutoa maini, utumbo, kwato nk. |
Taratibu za uchunaji wa ng’ombe zikiendelea. |
Nyama ya ng’ombe aliyechinjwa kwa mashine kwa ajili ya majaribio ikiwa tayari kwenda kwa mlaji. |
Jengo la machinjio ya kisasa Viungunguti linavyoonekana kwa nje. |
Kunenge ameyasema hayo jana katika ziara aliyofanya na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama katika machinjio ya kisasa Vingunguti Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa machinjio hayo ya kisasa yanatekelezwa kwa usimamizi wa Serikali na kwamba hatua iliyofikiwa ya majaribio ya uchinjaji wa mifugo ni ya kutia moyo ingawa bado kuna kazi kubwa inatakiwa kufanywa ili kukamilisha machinjio hayo mapya kwa wakati.
Amesema nyama itakayochinjwa katika machinjio hayo itakuwa ni ya kisasa inayowezwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kitoweo kwa kuwa imezingatia vigezo vyote muhimu vya afya.
“Ni kazi kubwa Serikali inathamini wananchi wake na inahakikisha inapata kitoweo kizuri, na kabla ya kuingia machinjioni mnyama anakuwa amepitia vipimo vyote ili kuhakikisha nyama haina madhara. Ni mradi mzuri na kwamba sasa yanafanyika majaribio ya mitambo iliyofungwa ndani ya machinjio haya ya kisasa Vingunguti,” Amesema Kunenge.
Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye machinjio ya kisasa Vingunguti ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni mkandarasi yamefanyika majaribio ya kuchinja mbuzi na ng’ombe.
No comments:
Post a Comment