Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 15 December 2020

BENKI YA CRDB YAENDELEA KUIBUKA KINARA KATIKA TUZO ZA MABENKI NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), akikabidhiwa tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020 .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwashukuru wateja kwa kuichagua Benki ya CRDB kuwa benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania (kushoto), Sanjay Rughani kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020.

Benki ya CRDB imeibuka na tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year) kwenye tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika Jumapili, 13 Desemba 2020. Tuzo hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Benki ya CRDB ilipoibuka kinara kwenye tuzo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kama Taasisi ya Fedha iliyoongoza kwa kuwasilisha Taarifa ya Fedha bora kwa mwaka 2018/2019 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka zikilenga kutambua ubora wa biashara mbalimbali kutokana na kura zinazopigwa na wateja wake. Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abudlmajid Nsekela amewashukuru wateja na Watanzania kwa ujumla kwa kuichagua Benki ya CRDB kama benki yenye asili ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year).

“Ushindi huu ni ishara tosha kuwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Benki yao ya CRDB na hivyo hii kwetu sisi ni deni ambalo tunapaswa kuwalipa kwa imani hii kubwa waliyotupa. Ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma bora zinazoendana na mahitaji ya wateja ambayo yamekua yakibadilika kila uchao” alisema Nsekela.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye tuzo hizo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe ameitaka sekta binafsi kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele gurudumu la uchumi wa nchi kwa kuwa sasa hivi wameshaelewa maono na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala ya uchumi.

“Wito wangu kwa wafanya biashara ni kuhakikisha wanazalisha bidhaa na huduma ambazo zitakidhi mahitaji ya soko la ndani lakini pia kuweza kushindana katika masoko ya nje na naamini uwezo huo tuko nao na sisi kama serikali tutaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara", Alisema Naibu Waziri Kigahe.

No comments:

Post a Comment