Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 22 November 2020

VODACOM KUGAWA ZAWADI ZA KUSISIMUA KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA UTOAJI HUDUMA NCHINI

  • Wateja kujishindia zawadi kemkem zenye thamani ya shilingi 3 bilioni katika msimu huu wa sikukuu.
  • Wateja kujishindia magari mapya 5, Pesa taslimu shilingi 1 milioni kwa wateja 25, muda wa maongezi na simu.
Mkurugenzi wa M-Pesa , Epimack Mbeteni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Shangwe Shangwena inayoendana na maadhimisho ya miaka 20 ya Vodacom na msimu wa sikukuu ambapo wateja wa M-Pesa watajishindia magari tano aina ya Renault kwid mpya na zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi 3 bilioni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa.
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa wakizindua rasmi promosheni mpya ya Shangwe Shangwena inayoendana na maadhimisho ya miaka 20 ya Vodacom na msimu huu wa sikukuu ambapo wateja wa M-Pesa watajishindia magari matano aina ya Renault kwid na zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi 3 bilioni.






Dar es Salaam, 21 Novemba 2020 - Mwaka huu Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali, Vodacom Tanzania PLC inasherehekea miaka ishirini ya utoaji huduma tangu ilipoanza kufanya kazi nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, kampuni hiyo imeongoza kuleta mabadiliko katika mifumo ya mawasiliano ya simu, mfumo wa malipo, na hivyo kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20, Vodacom Tanzania PLC imezindua kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama "Shangwe Shangwena" ambapo kupitia kampeni hii, Vodacom itawazawadia wateja wake ambao wamejikita zaidi katika mtindo wa maisha wa kidijitali kwa kutumia mfumo wa malipo ya kijanja wa M-Pesa.

Wateja hawa zaidi ya 15 milioni, watajishindia zawadi zenye thamani ya Shilingi 3 Bilioni zikiwemo magari mapya 5, zawadi za pesa taslim, rejesho la fedha pindi mteja anapolipia bidhaa au kutuma hela kupitia M-Pesa, MB za bure, muda wa maongezi, jumbe fupi (SMS) pamoja na punguzo la bei pindi mteja anapofanya manunuzi ya simu janja kwa kutumia M-Pesa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC Linda Riwa alisema kwamba anajivunia hatua ambayo Vodacom imefikia katika miaka ishirini iliyopita kwa kukuza maisha ya kidijitali nchini.

"Maono yetu ya kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali kupitia teknolojia sasa yanathibitika, kwani ubunifu wa bidhaa na huduma zetu umeleta matokeo chanya kwenye jamii kwa mfano mfumo wa malipo ya M-Pesa, suluhisho kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kupitia Lipa kwa Simu, mikopo kupitia M-Pawa na Songesha, Vodacom imebadilika kutoka kampuni ya mawasiliano tu na kuwa mwezeshaji wa maendeleo ya kiuchumi katika jamii,” alisema Bi Riwa.

Kampeni ya Shangwe Shangwena itawazawadia wateja zawadi mbalimbali na ofa maalum, zitakazowawezesha kufurahia huduma za mawasiliano wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni aliwashukuru wateja kwa uaminifu wao kwa miaka 20, na pia kwa kupokea maendeleo ya kiteknolojia na kusema kuwa msimu huu kampuni hyo inataka kusherehekea pamoja na wateja wake kupitia kampeni hii ya Shangwe shangwena.

“Wateja wanapata nafasi ya kushinda, wakati wowote wanapotumia huduma za M-Pesa kwa kufanya moja au yote kati ya haya; kufanya miamala ya fedha kati ya mtu na mtu (P2P), malipo ya biashara kupitia Lipa kwa Simu, Kuhamisha pesa kutoka Benki kwenda M-Pesa (B2C), Malipo ya huduma kama vile Luku, Dawasco nk, pamoja na ununuzi wa vifurushi, muda wa maongezi na simu janja au vifaa vya simu,” aliongeza Mbeteni.

Mbeteni aliwahimiza wateja kuendelea kutumia huduma tofauti za kidijitali kutoka Vodacom ili wajiongezee nafasi ya kushinda zawadi kemkem na za kufurahisha zinazotolewa wakati wa msimu huu wa sikukuu.

Kuhusu Vodacom:

Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawsiliano kwa zaidi ya wateja milioni 15.5. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.vodacom.co.tz

No comments:

Post a Comment