Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 3 March 2020

DSTV YAJA NA ‘JIONGEZE TUKUONGEZEE’



3 Machi 2020: Wateja wa DStv wanaendelea kufurahia ofa kabambe zinazotolewa na MultiChoice na sasa imezindua kampeni mpya ya ‘Jiongeze Tukuongezee’ ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huunganishwa na kifurushi cha juu zaidi bila malipo ya ziada.

Kwa kampeni hii mpya iliyoanza rasmi tarehe 1 Machi 2020 na ambayo itaendelea hadi mwisho wa mwezi Aprili 2020, mteja wa kifurushi cha DStv Bomba Tsh 19,000, akilipia cha ju yake ambacho ni Family Tsh 29,000, moja kwa moja ataunganishwa kifurushi cha Compact – Tsh 44,000 bila malipo ya ziada. Hivyohivyo mteja wa kifurushi cha DStv Family akilipia Compact, atapandishwa kwenda Compact Plus Tsh 84,00 wakati yule wa Compact akilipia Compact Plus ataunganishwa kifurushi cha juu kabisa cha Premium cha Tsh129,000.

“Kampeni hii ya Jiongeze Tukuongezee inaenda sambamba na mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa wateja wetu kote nchini wanapata maudhui bora na mengi kadiri iwezekanavy kwa gharama nafuu kabisa amesema Hilda Nakajumo – Mkuu wa Thamani kwa Wateja wakati wa uzinduzi rasmiwa kampeni hiyo uliofanika katika ofisi za MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Hilda amesema wanatambua kuwa kwa sasa wateja wana uzoefu na ufahamu wa maudhui bora na ya hali ya juu yanayopatikana kwenye vifurushi vya juu vya DStv, hivyo wameona ni vyema kuwapa wateja fursa ya kufurahia maudhui hayo kwa gharama nafuu.


No comments:

Post a Comment