Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 14 February 2020

WATEJA WA VODACOM KUFURAHIA MAWASILIANO YA KIWANGO CHA JUU BAADA KAMPUNI YA VODACOM KUBORESHA MENU NA HUDUMA ZAKE

Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” iliyofanyika hivi karibuni ambapo wateja wa Vodacom watapata vifurushi vya bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE kwa kupiga namba *149*01# . Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja wa Kampuni hiyo, Celvin Mmasy.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo wateja watapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE kwa kupiga namba *149*01#. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom, Celvin Mmasy. 
Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom Tanzania, Celvin Mmasy (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo wateja watapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha kwa JIMWAGE kwa kupiga namba *149*01# . Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.
  • Menu rahisi, na iliyoko wazi zaidi 
  • Bando mpya ya siku 3 za sauti na data ambazo zinatoa thamani zaidi kwa wateja 
13 Februari 2020, Dar es Salaam: Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza Tanzania Vodacom Tanzania PLC imetangaza kupunguza bidhaa zake katika menu yake kwa asilimia 75 katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja.

Akiongea wakati wa kutoa tangazo hilo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Bi Harriet Lwakatare amesema kwamba hatua hii ni mwitikio wa mahitaji ya wateja ambao walipendekeza kuwa menu iliyopita ilikuwa ni ngumu kuifuata kutokana na kuwepo kwa chaguzi nyingi.

“Tunakusudia kutoa huduma rahisi na zilizoko wazi kwa wateja wetu na menu hii iliyorahishwa inahakikisha kwamba wateja wetu wanaweza kwenda haraka na kwa hatua chache kufikia huduma wanayoihiji” alisema.

Wateja wa Vodacom wanapata huduma na bidhaa za kampuni kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo USSD code ya*149*01#, app ya Vodacom na tovuti ambazo sasa vinatoa chaguzi bora zaidi.

Kwa upande wake, Bi Linda Riwa, Mkurugenzi wa Idara ya Bishara wa kampuni ya Vodacom amesema “Sisi pia tumesikia kile ambacho wateja wetu wanahitaji.

Nina furaha kubwa kutangaza kampeni yetu mpya ya ‘Wajanja hatuzimi data” inayowapa wateja wetu unafuu katika matumizi ya intaneti pamoja na uzinduzi wa bando mpya ya Jimwage ambapo wateja wanaweza kupata GB 3 kwa siku 3 kwa shilingi 2,500 tu. Hii inawezesha kila mtu kutumia mtandao wetu Supa kwa bei nafuu na kufaidika zaidi.

“Pia tumeboresha huduma yetu ya sauti ili kuwezesha wateja wetu kuongea na wapendw wao bila kujali mtandao gani unayoipigia au gharama za ziada kwa mfano huduma yetu ya cheka iliyoboreshwa inatoa dakika 25 kwa shilingi 500 kupigia mitandao yote”

Akizungumza kuhusu bidhaa za Data, Mkuu wa Idara ya bidhaa za wateja Celvin Mmasy alisema, “uzinduzi wa bidhaa mpya za data zinawezesh kila Mtanzania kuungnishwa kupitia mtandao Supa wa Vodacom yenye uhakika, sidi kubwa kwa bei hafuu”.

Kuhusu Vodacom:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa zaidi ya wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu ya: www.vodacom.co.tz

No comments:

Post a Comment