Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akiangalia kazi za wabunifu wa mitindo wakati wa semina ya Ubunifu na Ufundi iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. |
Mbunifu wa mavazi, Doris Mbwilo (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakati wa maonesho ya kazi za ubunifu na ufundi za wajasiriamali. |
Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia), akizungumza na mbunifu wa mavazi, Doris Mbwilo, wakati wa maonesho ya bidhaa za ubunifu na ufundi. |
Baadhi ya wabunifu wa mitindo walioshiriki semina ya Ubunifu na Ufundi. |
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard, akizungumza na wajasiriamali wa kazi za ubunifu na ufundi. |
Ametoa wito kwa wajasiriamali hao kuyashika na kuyatendea kazi mafunzo waliyoyapata ili kuweza kufanikiwa katika malengo yao ya kukuza biashara zao kwa kuzifanya zenye kuaminika.
Amewataka kufungua akaunti za benki kama vile FANIKIWA zitawawezesha kulinda biashara zao na kuwafanya kuaminika na benki ili kuingia kwenye mfumo wa kibenki kupata mikopoa ambayo itawawezesha kukuza biashara zao.
“Kuna mambo matatu mnayokwenda kufundishwa, moja ni umuhimu kuwa na akaunti, pili umuhimu wa mauzo ya bishara zako kupitia kwenye akaunti zenu na tatu ni faida ya kuweka akiba katika kukuza biashara zenu.
“Mkiwa na mahesabu yanayoeleweka kwenye akaunti zenu ni rahisi kupata mikopo ya kibenki kuinua biashara zenu ili muweze kujiimarisha zaidi. Ubunifu mlionao kama mnaweka malengo na kuyasimamia na kuwa na mtiririko wa matumizi ya fedha yanayoeleweka mtaweza kuzilinda biashara zenu na kukuza ubunifu mlionao.”amesema Zaipuna na kuongeza kuwa.
“NMB imeamua kuwafikia wajasiriamali wadogo kada ya ubunifu kwani ni kada iliyosahaulika katika jamii katika uwezeshwaji, sisi tunaamini kuwa Ubunifu na Ufundi ni nguzo ya Uchumi hivyo tunadhamira ya dhati ya kuimaraisha Uchumi wa wajasiriamali wabunifu kupitia mafunzo na mikopo ya kibenki ambayo itatolewa.”amesema.
Kwa upande wa mtoa mada, Meneja wa wafanyabiashara wadogo wa NMB, Beatrice Mwambije ametoa wito kwa wajasiriamali hao kutambua kuwa kuna gharama ya kulipia ili kuweza kupata mafanikio wanayoyahitaji katika kazi zao.
“Katika biashara yoyote ni muhimu sana kuwa na akaunti ili kuweza kutunza kumbukumbu zako za manunuzi, mauzo na matumizi ili kukujengea uwazi na uwaminifu kwa benki kukupa mkopo utakao kuwezesha kukua katika biashara yako.
“Lakini katika mafanikio yoyote yale lazima kuna gharama ya kulipia ili uweze kuyafikia, unahitaji kuwa na watu sahihi ambao watakutoa sehemu moja hadi nyingine nao ni watu sahihi ambao fikra zao ni chanya na wakomavu zaidi.”amesema Mwambije.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Ubunifu wa mavazi ‘Speshoz Tanzania’ Jeffrey Jessey amewataka washiriki wa semina hiyo kuwa mstari wa mbele kujifunza vitu vipya, kuchangamana na watu na kuwekeza zaidi kwa kile wanachokipa ili waweze kufika mbali katika tasnia ya Ubunifu na Ufundi.
Kwa Upande wa washiriki wa semina hiyo wametoa kongole kwa NMB kwa kuwajali na kuwapa elimu ambayo itawatoa walipo na kupiga hatua zaidi katika kazi zao,
“Nimefurahi sana kuwepo hapa leo, mafunzo haya ni kitu kikubwa sana kwetu sisi wabunifu wachanga katika kupiga hatua zaidi, tumejifunza mambo mengi na mazuri ambayo tukiyatendea kazi basi naamini tutafika mbali zaidi,”amesema Addam Mtaullah Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Nguo Mbezi Luis (UMANGUMBE).
“Kwanza niwapongeza NMB wametuletea jambo sahihi kwa wakati sahihi, lakini pia mafunzo tuliyopata hapa yametufungua akili kujua jinsi gani tunaweza kutumia njia za kibenki kukuza biashara zetu kwa kuwa na akaunti unaiweka pesa yako salama.”amesema Doris Mbwilo mshiriki wa semina hiyo.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment