Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 4 March 2019

BENKI YA NBC KUIMARISHA UHUSIANO WAKE NA JESHI LA MAGEREZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, (kushoto), akiagana na Mkuu wa jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, (wa pili kulia), akizungumza na Mkuu wa jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike, (katikati) wakati alipomtembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya NBC na Jeshi hilo. Kushoto kwa Theobald Sabi ni Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wa Makampuni, Linley Kapya, pamoja na maofisa kutoka jeshi la Magereza.
Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wa Makampuni, Linley Kapya (wa pili kulia), akizungumza na Mkuu wa jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike, (katikati) wakati uongozi wa Benki hiyo walipotembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya kuangalia njia bora za kudumisha Mahusiano baina ya NBC na jeshi hilo. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, pamoja na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe pamoja na maofisa wa jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya NBC, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wa Makampuni, Linley Kapya na kulia kwake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama, pamoja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Mhandisi Tusekile Mwaisabila. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hive karibuni.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji Mhandisi Tusekile Mwaisabila akizungumza na Uongozi wa Benki ya NBC pamoja na Mkuu wa jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike katika hafla hiyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike pamoja na Mkurugenzi ya NBC, Theobald Sabi, (watatu kushoto) akipiga picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya NBC pamoja na maofisa wa jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment