Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 14 February 2019

UZINDUZI WA MALORI WA KUSTAJAABISHA ZAIDI KATIKA KANDA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kwenye picha kutoka kulia ni Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim na mwisho kushoto ni Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo na Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter.
Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea (wa kwanza kushoto ) akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kutoka kulia ni Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim.
  • Mercedes-Benz inapeleka mbele historia ya malori yenye nguvu nchini TANZANIA
  • Malori yote mapya aina ya Actros na Arocs yamezinguliwa 
Tarehe 8/02/2019 Jijini Dar es salaam - Actros mpya kabisa: Ni malori ya kuaminika na yenye ufanisi kwaajili ya masafa marefu na usamabazaji yamezinduliwa leo katika mji mkuu wa Tanzania.

Akiongea katika hafla hiyo ya kupendeza, Mkurugenzi wa Mauzo na Huduma kwa Wateja wa Malori ya Mercedes Benz Afrika Bwana Mr Torsten Bauerheim akisema, 'Malori yote mapya ya Actros na Acros yanakuja na injini yenye ufanisi yenye silinda 6 katika mstari, vyumba vya dereva vya kisaa vinavyoruhusu hewa kupita na Mercedes PowerShift 3 ya kisasa, injini ya kujiendesha yenyewe zikiwa na miundo mbalimbali tofauti kutegemeana na mazingira ya kanda husika. Aliongeza kuwa, Malori yote mapya ya Actros ni ya kuaminika na ya uhakika kwaajili ya ujenzi na matumizi katika barabara za vumbi na zote zimepitia majaribio makali ya ubora ya zaidi ya kilomita milioni 60 kabla ya kufanya uzinduzi wa soko.

Mkurugenzi Mtendaji wa wasambazaji walioithibishwa wa Mercedes-Benz, CFAO Motors Tanzania Ltd, Bwana Marius Prinsloo amesema kwamba 'Malori mapya ya Actros na Arocs yanatoa kiwango cha ziada cha uimara, ufanisi katika matoleo ya malori ya Mercedes-Benz Yakiwa yametengenezwa katika kiwanda cha malori kikubwa kuliko vyote duniani nchini Ujerumani, Malori haya yanakuja katika aina mbalimbali mahususi kwaajili ya soko letu la Tanzania - yakiwa yamebuniwa na kutengenezwa kuhimili mazingira magumu ya uendeshaji.

Yamejaribiwa kwa kina duniani kote, katika barabara za aina zote na katika mazingira magumu zaidi, magari haya ni mifumo bora zaidi kwaajili ya kazi ngumu. Majaribio yalijumuisha jumla ya zaidi ya kilometa milioni 6 za mbio za ustahimilivu zilizofanywa na kituo cha majaribio ya malori ya Mercedes-Benz nchini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Aliongeza kuwa 'Chumba kipya cha pekee cha dereva kinajivunia kiwango cha juu cha vifaa na mazingira mazuri ya ndani, wakati uendeshaji ni rahisi na wakustarehesha . Aina zote mbili za malori ya Actros na Arocs zinavutia kwa teknolojia ya kisasa zaidi na mfumo wa kuaminika wa uendeshaji kutokea chanzo kimoja. Injini zenye ustahimilivu, zenye nguvu na zenye ufanisi zinapatikana katika aina za utoaji moshi wa Euro III, IV na V, ikiwa inatoa aina mbalimbali za nguvu ya msukumo kuanzia 240 kW (326 hp) mpaka 460 kW (625 hp). Ikiwa imeunganishwa na toleo la hivi karibuni la Mercedes PowerShift 3, gia boksi ya kujiendesha yenyewe, malori ya Actros na Arocs yanafikia kiwango cha juu cha ufanisi wa mafuta, ikiwa inachangia kuongeza faida za uendeshaji

Actros mpya zimetengenezwa kwaajili ya usafirishaji wa masafa marefu pamoja na usambazaji wa mizigo mizito. Zinapatikana na mpaka aina 22 tofauti za chumba cha dereva na zinakuja katika matoleo ya chuma au ya kushikiliwa na upepo. Kwaajili ya mazingira magumu ya uendeshaji, Actros zinapatikana katika injini zenye nguvu za 15.61 na kasi ya 16 na gia boksi ya kujiendesha yenyewe ya Mercedes PowerShift 3

'Arocs mpya ya kustaajabisha iko kwaajili yako pale utakapo kuwa unahitaji ustadi wa kipekee - iwe katika shughuli za ujenzi mbali na barabara za lami. Malori ya Arocs yenye ustahimilivu mkubwa yanaweza kufanya kazi katika mazingira magumu zaidi ya barabara za vumbi mbali na bara bara za lami. Arocs zinapatikana kama Chassis-, Mixer-, Tipper- na aina mbalimbali za uendeshaji - kuanzia miundo ya 4x2 mpaka 8x8 na uzito (GCW) wa mpaka kufika tani 250.

Kwa kudokeza, Actros na Arocs yanaweka viwango vipya pale inapokuja kuhusu suala la usalama na mifumo ya usaidizi, inayomsaidia dereva na kuokoa maisha. Bwana Torsten Bauerheim alihitimisha.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Mercedes- Benz wasiliana na:

Jerome Sentimea
Simu: +255 754 422 000
Barua pepe: jsentimea@cfao.com

Or

http://www.media.daimler.com na http://www.mercedes-benz.com

No comments:

Post a Comment