Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 5 December 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA ARUSHA. DESEMBA 2, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200 kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha.
Continue Reading

No comments:

Post a Comment