| Mkurugenzi wa wateja wadogo wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko, Sarah Laiser (kushoto), na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Alina Maria Kimaryo wakikabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje (kulia), ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika sokoni hapo juzi, NBC ilikabidhi pia tanki la maji vizibao kwa ajili ya baba na mama lishe na watoza ushuru pamoja pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wafanyabiashara sokoni hapo. |
No comments:
Post a Comment