Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 2 November 2018

MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na zawaadi wakala bora kwa mwaka 2018 Kanda ya Dar es Salaam kwenye semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho (mbele) akiwasilisha mada kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa mawakala wa NMB akiuliza swali kwenye semina hiyo.
Benki ya NMB imetoa semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa NMB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.

Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala wa NMB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi katika kumuhudumia mteja.

Alisema NMB ndio benki pekee yenye idadi kubwa ya mawakala zaidi ya 6,000 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 228 na mashine za ATM zaidi 800 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.

Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.

Akiwasilisha mada za mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia watanzania. Alisema malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.

No comments:

Post a Comment