Mwanza, Tanzania, Novemba, 2018 - Benki ya I&M kupitia sera yake ya kurudisha kwa jamii “Corporate Social Responsibility” leo imetoa msaada wa Shilingi Milioni 10 ili kuboresha huduma katika wodi ya watoto ya Hospitali ya Sekou Toure ya Jijini Mwanza. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha hizo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.John Mongella, Mkuu wa Idara ya Wateja wa Reja Reja wa Benki ya I&M, Bi. Ndabu Swere amesema Benki ya I&M inautazama Mkoa wa Mwanza kiupekee katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na hivo uwepo wa Benki ya I&M utautaongeza nguvu ya mkoa huu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia utoaji wa huduma za kibenki kwa wateja wa reja reja, wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa.
“Wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi letu la Mwanza mnamo mwezi Mei, tulimuahidi Mkuu wa mkoa kuwa Benki ya I&M haitoishia tu katika kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wa Mwanza bali itajikita pia kuhakikisha kuwa inachangia katika ustawi wa jamii ya watu wa Mwanza kupitia sera ya kurudisha kwenye jamii ambapo kwa kudhihirisha hilo siku ya leo Benki ya I&M itakabidhi mchango wa Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kuboresha huduma katika wodi ya watoto katika Hospitali hii ya Sekou Toure” alisema Bi. Ndabu Swere
“Kama mnavyofahamu, serikali hii ya awamu ya tanoimejidhatiti kuhakikisha nchi inaenda katika uchumi wa viwanda. Lakini hatuwezi kwenda katika uchumi wa viwanda ikiwa hatuna nguvu kazi ya kutuwezesha kuendesha viwanda hivi. Hivyo kwa kuboresha sekta ya afya na kuzuia vifo vya watoto Taifa litapata nguvu kazi ambayo itatuwezesha kufikia matarajio ya uchumi wa viwanda” alisema Mh. Mongella.
Kuhusu Benki ya I&M
Benki ya I&M iliingia nchini Tanzania mwaka 2010 baada ya kuinunua iliyokua ikijulikana kama Benki ya CF Union ambayo ilianzishwa mwaka 2001. Katika kipindi cha miaka 8 tangu kuingia nchini, Benki ya I&M imeendelea kukua zaidi na kuweza kufungua matawi mapya 6 kutoka matawi mawili yaliyokua chini ya CF Union na hivyo kufikia jumla ya matawi 8. Matawi ya Benki ya I&M yanapatikana Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Benki ya I&M ni miongoni mwa Benki kongwe zaidi ikiwa imeanzishwa nchini Kenya mnamo mwaka 1974 na kusajiliwa katika soko la hisa la jijini Nairobi. Kwa sasa Benki ya I&M ina matawi katika nchi za Kenya, Rwanda, Tanzania na Mauritius.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Emmanuel Kiondo
Meneja Masoko na Mawasiliano
Benki ya I&M Tanzania
+255 743 858051 / +255 683 365014
No comments:
Post a Comment