Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 14 November 2018

FASTJET KUMILIKIWA NA WATANZANIA

Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Shirika la Ndege Fastjet Tanzania, Lawrence Masha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam hivi karibuni kuhusu uteuzi wake wa kuwa mwenyekiti wa shirika hilo. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kuhusu uteuzi mpya wa Mwenyekiti Mpya wa Fastjet Tanzania Lawrence Masha. Pichani wengine ni Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Fastjet Tanzania, Lawrence Masha na Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.
12 Novemba 2018, Dar es salaam - Kati ya mashirika ya ndege zinazokua kwa kasi zaidi, Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, leo imethibitisha mikakati ya kumiliki shirika hilo yanaenda vizuri.

Tarehe 6 Novemba Fastjet ilimteua Ndugu Lawrence Masha kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kwanza wa shirika hilo. Uteuzi huu umedhibitisha nia ya kuendelea kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi kama kampuni inayomilikiwa na Watanzania pamoja na masoko ya talii za nje.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Ndugu Masha alisema, “ tumejikita zaidi kwa watanzania ambao wamefaidika kutokana na huduma zetu kwa miaka sita sasa. Tunatarajia kuongeza kuongeza safari za ndani na pia kuongeza idadi ya ndege ambazo zinakidhi mahitaji ya soko”. Tunaona fursa kufanya kazi na kushirikiana na mashirika ya ndege za ndani na nje ya nchi pamoja na Air Tanzania kutimiza mikakati ya serikati ya utalii.

Ndugu Masha ataendeleza vizuri na mikakati ya kubadilisha shirika hilo pamoja na uongozi kuhakikisha wanatoa huduma kwa watanzania.

Fastjet imetoa huduma kwa miaka sita ambapo imesafirisha zaidi ya abiria milioni 2.5 ndani ya Tanzania pekee.

Shirika hili lenye bei nafuu lina hudumia usafiri wa ndege katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe. Na linarekodi ya kusafirisha wastani wa abiria 30,000 kwa mwezi.

Kuhusu Fastjet:

Fastjet ni shirika lenye tuzo mbalimbali (Kama Skytrax World Airline Awards Best Low-Cost Airline in Africa 2017 na Leading African Low-Cost Carrier, World Travel Awards 2016 and 2017 ) Shirika hili lililoanza shughuli zake Tanzania mwaka 2012, kwa kusafirisha abiria kati ya Dar es salaam na Kilimanjaro na Mwanza pekee. 

Leo, Fastjet inasafirisha abiria ndani ya Tanzania kati ya Dar es salaam na Mbeya, Kilimanjaro na Mwanza huku ikiwa na safari za kimataifa kutoka Tanzania kwenda Harare, Zimbabwe na Lusaka, Zambia. 

Fastjet ilianza safari za ndani ya nchi ya Msumbiji kati ya Maputo na Beira, Nampula na Tete Tarehe 3 Novemba 2017 na pia ilisherehekea mwaka wake wa pili wa kufanya shughuli zake ndani ya Zimbabwe mwaka jana. Shirika lnafanya shughuli zake kati ya Harare na Victoria Falls, Harare Dar es salaam na Kutoka Harare na Victoria falls kwenda Johanesburg, South Africa.Shirika hili tayari limeshasafirisha zaidi ya abiria Milioni 3, huku likiwa na rekodi nzuri ya kutua na kuondoka kwa wakati na kujijengea sifa ya kuwa shirika la ndege la kuaminika na nafuu.

No comments:

Post a Comment