Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 5 October 2018

VODACOM YASHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akimhudumia mteja Rafi Soule, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Mteja katika duka la Vodacom lililopo makao makuu ya kampuni hiyo Morocco jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja (Customer Care) Harriet Lwakatare.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kushoto) akizungumza na wateja wa Vodacom alipotembealea duka la Vodacom lililopo Morocco jijini Dar es salaam kuwashukuru wateja wa kampuni hiyo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja (Customer Care) Harriet Lwakatare na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
WATEJA WA KWANZA KUNUNUA LINE YA VODACOM: Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja (Customer Care) Harriet Lwakatare (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa kwanza kununua laini ya simu ya Vodacom mwaka 2000, Mama Sion Nnko, wakati mtandao huo unaanzishwa. Wateja hawa walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Sambamba na zawadi hiyo wateja hao walizawadiwa TUZO points zenye thamani ya 200,000 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja. Kushoto ni Benedict Kajukano, Bernard Masao na Emmanuel Lutashohyce.
Baadhi ya wateja wa kwanza kununua laini ya simu ya Vodacom mwaka 2000, kutoka kushoto Sion Nnko, Benedict Kajukano, Bernard Masao, Emmanuel Lutashohyce na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja (Customer Care) Harriet Lwakatare wakimsikiliza Afisa chapa wa kampuni hiyo, Grace Kijo wakati walipotembelea Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.

No comments:

Post a Comment