KAMPUNI ya moja Beti inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha imeutambulisha mchezo mpya wa kubahatisha Jijini Mbeya, unaofahamika kwa jina la ‘BOOM PESA’, na kuwataka wakazi wa Mkoa huo kujitokeza na kununua tiketi ili waweze kujishindia fedha taslimu papo hapo.
Akizungumza leo Jijini Mbeya wakati wa kuutambulisha mchezo huo wa kubahatisha, Msimamizi wa kituo cha huduma kwa Wateja kutoka Moja Beti Florida Mwangosi, amesema mchezo huo ni mpya lakini ni rahisi sana kupata fedha tofauti na michezo mingine .
“Huu mchezo wetu wa kubahatisha unaofahamika kwa jina la Boom Pesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea” Alisema Florida Mwangosi .
Naye Balozi wa Boom Pesa Sabrina Ibrahimu, alisema mwitikio kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye mchezo huo wa kubahatisha ni mkubwa sana , nakwamba wananchi zaidi ya 100 kwa siku moja walijitokeza na kushiriki mchezo huo .
“Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuupokea huu mchezo wetu mpya wa kubahatisha, nawapongeza sana maana wamekuja na baadhi wameshinda tunawashukuru sana tunawaomba waendelee kuucheza mchezo huu” Alisema Sabrina Ibrahimu .
Aidha Baadhi ya washindi wa Boom Pesa kutoka Jijini Mbeya ambao ni Yasinta Ndesabula na Taison John waliliambia gazeti hili kuwa ni mchezo ambao wao hawakutegemea kama wangecheza na kushinda, ambapo wamewahimiza watanzania wengine kucheza ili waweze kujishindia fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment