Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, Dk Peter Kilima (kushoto), wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mjini Dodoma hivi karibuni. Katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto) alisema benki hiyo ilidhamini mkutano huo wakiwa kama wadau wakubwa wa serikali za mitaa hii ikitokana na DCB kuanzishwa na manispaa za Jiji la Dar es Salaam na pia kupata fursa ya kuwajulisha manispaa nyingine na wananchi kuwa benki hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi hasa wenye kipato cha chini. |
No comments:
Post a Comment