Wamiliki wa Mabasi ambao ni wanachama wa TABOA. |
“Tunaona uwezo mkubwa sana kwenye magari ya usafirishaji abiria na pia ya mizigo. Huduma hii mpya ya bima inatupa nafasi ya kipekee kukuza biashara yetu kwa upande mmoja na kwaupande mwingine kuwarahisishia malipo wateja wetu,” bwana Rahim Kanji, Meneja Mkurugenzi wa NIC kitengo cha biashara alisema.
“Kusisitiza umuhimu wa huduma hii, tumeweka timu maalamu kusimamia utoaji wa huduma hii kwa wamiliki wa basi nchini kote,” aliendelea kusema.
“Mkutano huu na TABOA ni hatua muhimu kama benki ya NIC tukiwa tunaendelea na mchakato mzima wakutoa huduma bora kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla ambazo zina boresha maisha yao. Benki yetu haiachi kutafuta namna za kueendelea kuboresha na kuzindua huduma mbali mbali zinazo timiza mahitaji ya aina tofauti,” aliongezea.
Mnamo mwaka wa 2009, Benki mama ya NIC (NIC Bank Group) ilinunua hisa katika benki ya Savings and Finance (S&F) Commercial Bank na kuibadilisha kwa mafanikio makubwa kuwa benki ya NIC Tanzania. NIC Bank Group ndio benki mama ya benki ya NIC Kenya, ambayo inamaffanikio makubwa sana Kenya ambapo ni benki ya 7 kwa ukubwa wa wanahisa naya 9 kwa ukubwa wa rasilimali.
NIC Bank Group imeendelea kukuwa kwakiasi kikubwa kadiri miaka inavyo enda na hii ikiwa sambamba na mpango wake endelevu wa “Kujenga mafanikio kwa pamoja” Benki ya NIC Tanzania inaweka msisitizo mkubwa kukuwa na wateja wake wenye biashara ndogo na zakati, biashara za nyumbani, wahitimu, na wakurugenzi wa mashirika makubwa.
Kupata huduma hii, mmiliki wa basi anahitaji tu kutaja malipo ya bima anayotaka, kiasi cha bima yake, jina la kampuni ya bima na idadi ya malipo aliopangiwa kufanya kila mwezi. Huduma hii mpya inaendana na bima za kipindi cha mwaka mmoja. Na pia huduma hii itawapa usalama watanzania wote barabarani maeneo yote nchini.
Ikiwa sehemu ya benki ya NIC kuendelea kuboresha huduma kwa wateja, benki hii imewekeza kwenye kutoa huduma bunifu na kuambatanisha ujuzi wake na matumizi ya teknolojia ya kisasa kuwaokoloea wateja wake fedha na mda.
Mapema mwaka huu, benki ya NIC ilizindua huduma ya NIC NOW, ambayo ni huduma ya fedha kwenye simu. Sambamba na hilo, benki ya NIC ilizindua huduma mbali mbali za kidijitali chini ya mwamvuli wa NIC Lipa mahususi kwa ajili ya wateja wa rejareja, biashara ndogo ndogo na benki za mashirika makubwa. Huduma hizi zinawawezesha wateja kufanya malipo kupitia huduma ya simu ya mkononi ya M-Pesa.
Benki ya NIC Tanzania ina matawi matano yaliopo Arusha, Mwanza na matatu Dar es Salaam mtaa wa Ohio, Samora na Kariakoo. Benki ya NIC Tanzania inajivunia kuwa na huduma nyingi za kifedha ambazo zote zinapatikana sehemu moja zikiwemo huduma ya fedha kwa ajili ya rasilimali, akaunti binafsi na biashara, akaunti za kuhifadhi, huduma za bima, kubadili hela za kigeni na huduma za fedha kwa mashirika na taasisi.
No comments:
Post a Comment