Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 23 October 2018

BENKI YA NBC YAZINDUA HUDUMA YA NBC KIKUNDI MOBILE MJINI MBEYA

Mkuu wa Kitengo cha Uhai wa Wateja wa Benki ya NBC Tanzania, Gaudence Shawa (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya NBC Kikundi Mobile katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya jana. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Hassan Mkwawa na Meneja wa NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo. NBC Kikundi Mobile hurahisisha uhamishaji wa fedha kutoka katika akaunti ya kikundi kwenda kwa mwanakikundi kwa kutumia simu ya mkononi na pia watia saini mpaka wanne wanaweza kuidhinisha miamala popote walipo kwa kutumia simu zao.
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Allen Masombola (kushoto), akitoa maelezo jinsi ya kutumia huduma ya NBC Kikundi Mobile ilipozinduliwa rasmi mjini Mbeya jana. NBC Kikundi Mobile hurahisisha uhamishaji wa fedha kutoka katika akaunti ya kikundi kwenda kwa mwanakikundi kwa kutumia simu ya mkononi na pia watia saini mpaka wanne wanaweza kuidhinisha miamala popote walipo kwa kutumia simu zao. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Hassan Mkwawa na kulia ni Meneja wa NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo. 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Hassan Mkwawa (katikati), akitoa hotuba ya uzinduzi wa NBC Kikundi Mobile jana mjini Mbeya.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya, Stella Kategile (kushoto) akizungumza na Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, William Kallaghe (wa pili kushoto), Mkuu wa Uhai wa Wateja wa NBC Tanzania, Gaudence Shawa (kulia) na Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Edwin Chrisant katika hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Hassan Mkwawa, akishikana mikono na Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo (kushoto) baada ya kuzindua wa huduma ya NBC Kikundi Mobile katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya jana. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhai wa Wateja cha NBC, Gaudence Shawa. NBC Kikundi Mobile hurahisisha uhamishaji wa fedha kutoka katika akaunti ya kikundi kwenda kwa mwanakikundi kwa kutumia simu ya mkononi na pia watia saini mpaka wanne wanaweza kuidhinisha miamala popote walipo kwa kutumia simu zao.
Meneja wa NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo (wa tatu kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakikabidhi vikombe kwa Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa NEEC, Anna Dominic (kulia), vitakavyopewa washindi katika vitengo mbalimbali walioshiriki maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na NEEC ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Kutoka kushoto ni, Allen Masombola, Jasmin Kilalile, Clara Kihaga na mwingine ni Edwin Chrisant kutoka NEEC. 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Hassan Mkwawa (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa NBC mara baada ya kuzindua rasmi NBC Kikundi Mobile mjini Mbeya jana.

No comments:

Post a Comment