Katika kutekeleza mpango huo, tayari Airtel imefungua maduka zaidi ya 400 katika maeneo mbalimbali Nchini na hivyo kusogeza karibu na wateja wake huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuma na kupokea pesa, kurudisha namba iliyopote, kuswap Sim Card na kununua vifurushi mbalimbali vya Airtel.
Akizungumzia mpango huo wa kufungua maduka na kutoa huduma kwa Mkoa wa dare s Salaam, Meneja wa Biashara Airtel Mkoa wa Dar es Salaam, Brighton Majwala amesema, miongoni mwa maduka yoa ya mkoa wa Dar es Salaam yamewezesha wateja wao kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi zaidi.
“Sisi Airtel, tumeamua kuanzisha maduka haya ili kusogeza karibu huduma zetu kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wateja wetu kupata huduma hizo kwa urahisi na pia karibu na maeneo yao,” amesema Majwala.
“Hata hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa mawakala wetu kuweza kupata huduma za Airtel Money na huduma nyingine bila kutembea umbali mrefu kuzifuata kama ilivyokuwa hapo awali”. ameongeza.
Kwa upande wao baadhi ya wateja na mawakala wa wa Kampuni hiyo, wameeleza namna ambavyo wananufaika na huduma zinazotolewa na maduka hayo ya Airtel katika maeneo yao.
“sisi wateja, tunafurahia huduma hizi kusogezwa karibu na maeneo yetu kwani inaturahisishia kupata huduma na kuokoa muda ambao tungeutumia kufuata huduma hizo maeneo mengine ya mbali na hapa” walieleza wateja hao.
“Mawakala wengi wa hapa maeneo ya Tangi Bovu tunanufaika sana na uwepo wa Duka hili la Airtel katika maeneo yetu kwani kwa sasa tuweza kumuhudumia mteja kiasi chochote cha Airtel Money bila kuhangaika kufuata floti maneo ya mbali” aliongeza wakala Elizabeth Madeje
Kufunguliwa kwa maduka hayo katika maeneo ya karibu na wananchi, kumeelezwa kuwasaidia wananchi na wateja wa Airtel kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi na hivyo kuokoa fedha na muda wa kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.
No comments:
Post a Comment