Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 18 August 2018

TANZANIA YATEULIWA RASMI KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA SADC

Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 mpaka Agosti 2019.

Kufuatia uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika mjini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali mjini Windhoek, Namibia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afika Kusini, Mhe Lindiwe Sisuli.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda, Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob.
Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini.
Waasisi wa SADC wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Tiafa wa Namibia na wimbo wa SADC ukipigwa, kushoto ni Rais mstaafu wa kwanza wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Sam Nujoma na kulia kwake ni Rais wa mstaafu wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano. 
Picha ya pamoja.
Bofya hapa kwa picha zaidi

No comments:

Post a Comment