Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 16 August 2018

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA LAFANYIKA SEOUL, KOREA

Mgeni Rasmi katika Kongamano la kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) akitoa hotuba ya ufunguzi, kwa niaba ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu: Kutoka kushoto: Makamu Mwenyekiti wa Korea-Africa Foundation (KAF), Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Geoffrey Mwambe, Balozi wa Tanzania Korea Mhe. Matilda Swilla Masuka, “Congressman” KIM Gyu-hwan, Rais wa KAF, Balozi Yeon-ho CHOI, na mwisho kulia ni Katibu Mtendaji wa Chama cha watengenezaji madawa (TAPI), Bw. Abbasi S. Mohamed. 
Picha ya Pamoja ikijumuisha meza kuu na watoa mada kutoka: TIC, TFDA, MSD, Korea Health Industry Development Institute (KHIDI) na “Korea Medical Devices Industrial Association”.
Ubalozi wa Tanzania uliopo Seoul nchini Korea kwa kushirikiana na “Korea-Africa Foundation” na “Korea Chamber of Commerce and Industry” uliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa wadau wa sekta ya Afya lililofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea. Kongamano hilo la aina yake, liliandaliwa ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha sekta ya Afya.

Kongamano hilo lililenga kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Tanzania, lilihudhuriwa na makampuni zaidi ya 100, kutoka pande zote mbili ikijumuisha: Makampuni ya utengenezaji madawa na vifaa tiba; Vyuo Vikuu; Taasisi za utafiti; Hospitali; Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Makampuni kutoka katika sekta binafsi; na Diaspora wa Tanzania waliopo Seoul.

Wakati wa Kongamano hilo, mada mbalimbali ziliwasilishwa zikijumuisha: Fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya utengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Mazingira ya ufanyaji biashara na vivutio “incentives” vinavyotolewa na Serikali; Hali ya soko na uhitaji (Market Potentiality); Taratibu za kufuatwa katika uingizwaji wa bidhaa za madawa na uanzishwaji wa viwanda husika; na Utayari wa sekta binafsi katika kushirikiana na wenzao wa Korea katika biashara na ubia katika viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Continue Reading

No comments:

Post a Comment