Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 10 February 2018

SAFIRI KIJANJA KWA KUTUMIA VIPENGELE VYA UBER MWONGOZO WA KULETA UFANISI KATIKA SAFARI ZAKO


7 Februari 2018 - Iwe unatumia Uber kwa mara ya kwanza, au mwenye uzoefu wa kutumia Uber, kuna uwezekano kwamba kuna vipengele ambavyo huvijui. Vifuatavyo ni baadhi ya vipengele ambalo yamkini huvifahamu, ambavyo vitarahisisha na kuleta ufanisi mkubwa kwenye safari zako za Uber.

Vituo vingi vya kusiamama - gari kusimama kwenye kituo unachotaka
Iwe uko kwenye safari kufanya shughuli zako za wikendi na ukataka kumchukua rafiki ukiwa safarini kuelekea uwanja wa ndege, au unarudi nyumbani baada ya dina na ungependa mwenzako ashukie njiani, ni rahisi kuliko kuwachukua na kuwashusha marafiki zako unapokuwa safarini. Uber ina kipengele kinachokurahisishia utaratibu wa kuongeza vituo vya kusimama barabarani, tafsiri yake ni kwamba huna haja ya kubadilisha mahali unakoenda unapokuwa safarini.

Ukitaka kutumia kipengele hiki, chagua safari yangu, gusa alama ya “+” iliyo karibu na “Unaenda Wapi” katika kisanduku cha mahali unakoenda ili uongeze vituo vya kusimama wakati wowote kabla au unapoendelea na safari zako. Pia unaweza kuongeza, kubadilisha au kuondoa mahali unakoenda kutoka kwenye skkrini ya safari iliyopo kwenye programu.

Huduma zinazopatikana ndani ya programu - tunatoa usaidizi masaa 24 kote ulimwenguni.
Wasafiri wanapata majibu ya maswali yao haraka kwa sababu wanaweza kutumia mfumo wa vituo vya usaidizi vinavyotoa usaidizi masaa 24 kote ulimwenguni.

Kama kuna tatizo lolote la kiufundi, au ulitozwa pesa nyingi au ulisahau mzigo ndani ya gari, unaweza kupata huduma zitakazokusaidia kutatua matatizo kama haya ndani ya programu katika sehemu ya huduma zinazopatikana ndani ya programu, huduma hizi zinapatikana ndani ya programu yako ya Uber kwa kugusa aikoni ya menyu (mistari mitatu) iliyo kona ya juu ya upande wa kushoto ya programu yako. Sasa unaweza kugusa aikoni ya "usaidizi" utelezeshe chini kisha uripoti tatizo husika.

Pongezi - Unaweza kumpongeza dereva kwa kutumia kitufe tu!
Uber inawapa wasafiri nafasi ya kuwashukuru na kutambua mchango wa madereva kwa kazi nzuri na weledi wao. "Unapotoa shukrani ㄧ kwa mfano, kwa weledi pamoja na dereva kujua barabara za jiji, au kwa sababu ya mazungumzo mazuri ㄧ ujumbe huu utaonekana kwenye skrini ya dereva ili kuwajulisha kuhusu shukrani uliyotoa," amesema Janet Kemboi, Afisa Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki.

Kuchati ndani ya programu - kurahisisha mawasiliano
Ubora wa safari unategemea jinsi msafiri atakavyochukuliwa, ndio maana tumejiongeza kwa kuweka kipengele kinachowasaidia wasafiri kuwasiliana na madereva ndani ya programu ya Uber.

Ili uweze kuchati na dereva anapokuwa njiani kuja kukuchukua, nenda kwenye mlisho wa Uber na uguse "wasiliana" kisha "chati." Dereva anapopokea ujumbe kutoka kwako atasomewa kwa sauti. Madereva wanaweza kukiri kwamba wamepokea ujumbe kwa kugusa mara moja tu kwa kutumia alama ya "bomba" kwenye programu yako.

Ratibu safari zako - panga mambo yako mapema
Iwe unawahi kwenda uwanja wa ndege, una mkutano unaotakiwa kuhudhuria, au unaratibu siku nzuri ya mtoko na mpenzi wako hutakuwa na wasiwasi woowte kuhusu usafiri utakaotumia. Unaweza kuratibu safari mapema kuanzia siku 30 hadi dakika 15 kabla ya safari yenyewe ili usikose mambo muhimu katika maisha yako.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi:
  1. Gusa aikoni ya gari ili uratibu safari.
  2. Weka tarehe, saa, mahali, ungependa kuchukuliwa sambamba na mahali unakoenda, aina ya safari, na utapewa makadirio ya nauli utakayolipa.
  3. Hakikisha maelezo ya safari uliyoratibu ni sahihi kisha uguse Ratibu. Badilisha au ufute maelezo haya wakati wowote kabla ya safari yako.
  4. Furahia safari yako - Tutakutumia ujumbe wa kukumbusha siku ya safari na kukuarifu gari likiwa njiani kuja kukuchukua. Pia tutakujulisha iwapo kutakuwa na mabadilko yoyote kwenye nauli.

Kumwitia ndugu usafiri
Sote tumejipata katika hali hii. Wakati ambao bibi yako anahitaji usafiri wa kumpeleka sokoni wakati wewe uko kazini. Au rafiki wa karibu anakupigia simu usiku kukuambia anahitaji usafiri wa kumfikisha nyumbani kutoka uwanja wa ndege.

Habari njema? Unaweza kuita usafiri kwa ajili ya ndugu au rafiki wa karibu moja kwa moja kwenye programu yako! Ukiweka mahali pa kuchukuliwa ambapo si mbali sana na mahali uko, tutakuuliza kama usafiri unaoita ni kwa ajili ya ndugu au rafiki. Kisha unaweza kuchagua jina la msafiri kutoka kwenye namba za simu kwenye simu yako, uweke mahali anakoenda, na umuitie usafiri.
             
Dereva akiondoka kwenda kumchukua, msafiri atatumiwa ujumbe wenye maelezo ya dereva na kiungo cha kufuatilia barabara anayotumia. Anaweza kuwasiliana na dereva moja kwa moja. Dereva ataona jina la msafiri na anaweza kuwasiliana na yeye moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment