Kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini Vodacom Tanzania
kupitia kampeni yake ya “Ukarimu wa
Vodacom” yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku imewafuturisha wakazi wa
Kiwanga wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Huduma hii yenye lengo la kuendeleza mshikamano inakwenda
sambamba na kuwawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla wao kujiunga na
kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE
wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma
hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili
kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando
kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine
linadumu kwa siku 7.
No comments:
Post a Comment