Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameipongeza Vodacom Tanzania Foundation kwa kuendelea kuwafuturisha watoto na wazee waishio katika mazingira magumu nchini.
Mh. Waziri Mkuu ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Ruangwa Lindi katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Huu ni mwendelezo wa kampeni ya “Ukarimu wa Vodacom” ambayo ina lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku.
Huduma hii yenye lengo la kuendeleza mshikamano inakwenda sambamba na kuwawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla wao kujiunga na kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.
No comments:
Post a Comment