Mkuu wa Kampuni ya
mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Mussa Baucha (kushoto)
akikabidhi msaada wa Saruji na Mabati
kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi
la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa
jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akizungumza na vyombo vya habari kabla ya kupokea
msaada wa Saruji na Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa
ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi
la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana katika mkoa huo ambapo Zantel
walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 vyote vikigharimu Sh. 13
milioni. Kushoto ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Mussa (Baucha).
Mkuu wa Kampuni ya
mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Mussa Baucha (kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa
kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi
la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel
walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13
milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya za mkoa huo mabati
yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa
mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana
kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 kwa
pamoja vilikabidhiwa na Kampuni ya Zantel. (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya
Chakechake Mhe. Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani
Mhe. Hemed Suleiman Abdallah.
No comments:
Post a Comment