Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 16 November 2016

BENKI YA POSTA YATOA MSAADA KWA JESHI LA POLISI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya (kushoto) akiongea na Waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya msaada huo, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande, Camillius Wambura.

Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande, Camillius Wambura (kulia) akitoa shukrani kwa Menejimenti ya TPB kwa msaada walioutoa, kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Jema Msuya.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya akimkabidhi kompyuta Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande, Camillius Wambura. TPB ilitoa kompyuta 2 na samani za ofisini zenye thamani ya shilingi 8m, ili kufanikisha jeshi kutimiza azma yao ya kulinda raia na mali zao ipasavyo. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Masuala ya Umma ya Benki hiyo, Noves Moses.

Picha ya Pamoja baada ya makabidhiano ya msaada: Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande, Camillius Wambura, Inspekta Aden Mwakyoma na Meneja Mwandamizi wa Masuala ya Umma ya Benki hiyo, Noves Moses.

Jumatano, Tarehe 16/11/2016 Benki ya Posta Tanzania (TPB) imetoa msaada wa kompyuta mbili (2) na samani za ofisi, vyote vina thamani ya sh. Milioni 8 kwa Jeshi la Polisi – Tanzania. Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande Camillius Wambura na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Jema Msuya.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Msuya alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ambayo jeshi hilo inaifanya, ya kulinda usamala wa raia na mali zao, na pia kulinda usalama katika sekta mbalimbali hususan sekta za kifedha. ‘Tunaamini vifaa hivi, vitaenda kusaidia huduma mbalimbali mnazozitoa kwa raia nchini na pia kuongeza ufanisi katika kazi zenu.’

Aliongeza kwa kusema kuwa ni vizuri hata taasisi nyingine nazo zikajitokeza kama wao ili kusaidia Jeshi la Polisi katika kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi, hususan katika swala la vitendea kazi.

Kwa upande wake Afande Wambura, alisema amepokea kwa furaha msaada huo kutoka TPB na utawasaidia sana katika shughuli zao za kila siku. “Tunaishukuru sana Benki ya Posta Tanzania kwa msaada huu, na tunaamini utatusaidia sana katika shughuli zetu za kila siku, hasa katika swala zima la kuweka kumbukumbu, ili kuboresha ulinzi wa raia na mali zao.” Alisema kuwa msaada huo ni mfano tosha kuwa Benki ya Posta inashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama ili kuboresha ustawi wa jamii nzima kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment