Mbogella amesema mwaka 2015 pekee zaidi ya shule 140 za msingi na sekondari zilipata zaidi ya madawati 7,000 kwa Tanzania nzima katika mpango wa kuendelea kutatua tatizo la madawati mpaka kufikia septemba 2016 tayari wametumia zaidi ya milioni 900. “Upande wa afya tumetoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika” alimalizia Augustino Mbogella.
Wakati huo, viongozi na wananchi wameombwa kutembelea banda la NMB ili kuweza kupata elimu zaidi likiwemo pia suala la ufunguaji wa akaunti mbambali kwenye benki hiyo ambazo zina manufaa makubwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la NMB kwenye maonyesho ya ALAT.
|
No comments:
Post a Comment