Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution, Mike Raymond akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa kusaini mkataba wa maelewano wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa katika bara zima la Afrika wakianzia nchini Tanzania na uzinduzi wa kadi mpya ya malipo itakayoitwa Mimosa Black Card. Kadi hii itaruhusu mteja kuweka na kutoa fedha bila ya kuhitaji akaunti ya benki.
Mike alisema kuwa kadi hii mpya ni sawa na kadi ya kawaida ya malipo ya kabla ila ni ya kipekee kwa sababu haiunganishwi na akaunti ya benki hivyo kuifanya kuwa ya gharama nafuu na pia urahisi wa kuweka na kutoa fedha. Kadi hii pia italindwa kwa neno la siri (PIN) na teknolojia ya juu ya ulinzi.
Watumiaji wa kadi ya Mimosa wanaweza kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM), kufanya malipo ya kutumia kadi katika maeneo yote yenye huduma hiyo na pia kufanya manunuzi mtandaoni mahali popote duniani kupitia mtandao wa Visa. Vile vile wateja wanaweza kuweka pesa katika kadi zao kupitia tawi lolote la UBA Tanzania au mitandao ya simu M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na pia katika akaunti za kukusanya fedha katika benki za CRDB na Exim.
|
No comments:
Post a Comment