Dar es salaam, Oktoba 1, 2015: Benki ya FNB Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujijengea mustakabali salama kifedha kwa kuendelea kuweka akiba zaidi benki kupitia fursa ya mpango mpya wa benki hiyo wa “Weka akiba na ushinde”.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha wakati akizindua mpango huo jijini Dar es salaam ambapo alisistiza umuhimu wa kuweka akiba. Mpango huo wa Weka Akiba na Ushinde utaanza tarehe 1 Oktoba na kuendelea mpaka mwisho wa Disemba 2015.
Ikiwa ni sehemu ya mpango huo utakaodumu kwa miezi mitatu, wateja waliopo na wateja wapya wataingizwa moja kwa kwenye droo kutokana na akiba ya kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao, kwahiyo watakaoweka akiba zaidi watapata nafasi ya kushinda shilingi milioni 5 ambazo zitatolewa kila mwezi kwa kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki.
Botha alisema, “Katika kuendeleza utamaduni wa benki hii kuwatunuku na kuwanufaisha wateja wake huku ikiendelea kutoa huduma za kisasa za kibenki, FNB inatoa fursa hii kwa wateja kuweza kujinufaisha kutokana na kuweka akiba huku wakijijengea mustakabali salama kifedha”.
No comments:
Post a Comment