Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 22 September 2015

WASHINDI ZAIDI WAPATIKANA KAMPENI YA AKAUNTI ZA MISHAHARA YA BENKI YA NBC

Meneja Malipo ya Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya wateja 50,000 wa zamani na wapya walishiriki na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa hadi asilimia 50 ya mishahara yao na huduma za bure katika baadhi ya miamala kupitia akaunti hizo. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GMT), Mrisho Millao, Meneja Akaunti za Mishahara, Deogratius Kibodya na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo.
Meneja Malipo ya Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (wa tatu kushoto), akibonyeza kompyuta ili kupata washindi wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya wateja 50,000 wa zamani na wapya walishiriki na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa hadi asilimia 50 ya mishahara yao na huduma za bure katika baadhi ya miamala kupitia akaunti hizo. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GMT), Mrisho Millao, Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo na Meneja Akaunti za Mishahara wa benki hiyo, Deogratius Kibodya.
Meneja Akaunti za Mishahara wa NBC, Deogratius Kibodya (kulia) akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya Mcheza Kwao ya benki ya NBC ambayo wateja wa zamani na wapya wenye akaunti za mishahara katika benki hiyo walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika mishahara yao na pia waliweza kupata zawadi ya kuondolewa ada watumiapo huduma za mobile banking za NBC kupitia akaunti zao za mishahara. Kushoto Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao na katikati ni Meneja Malipo ya Mishahara wa benki hiyo, Amos Lyimo.

No comments:

Post a Comment