| Vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga, Jijini Dar es Salaam wakishangilia baada ya Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya alipokabidhi msaada wa mashine tatu za kufyatulia matofali kwa Mlezi wao, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Rev. Richard Hananje anayelea takribani vijana 150 hivi. Shirika limetoa msaada wa mashine hizo tatu za kufyatulia matofali ya kufungamana zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kwa vijana hao na mtaji ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato na kusahau utumiaji wa madawa ya kulevya. |
No comments:
Post a Comment