Wateja watakaonunua bidhaa za LG katika kipindi hiki cha ramadhani na Sabasaba watafurahia punguzo la bei la hadi asilimia 15 pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo zawadi za bure, alisema Meneja mwandamizi wa LG, Mr. Kim Taehoon.
Mr. Kim pia alitumia fursa hiyo pia kuitambulisha friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” kwa mara ya kwanza kabisa katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini.
Alisema friji hiyo ina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa kuzuia bakteria na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama na wa kiafya, friji ina makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, aina hii ya milango huja pamoja na kioo imara. Friji hii inatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter Compressor” ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha maonyesho ya biashara ya Sabasaba, wateja wa LG watajipatia ofa kabambe pale watakapotembelea banda la LG kiwanjani hapo ambapo pia wataweza kupata bidhaa nyingine mbalimbali za LG ikiwemo friji jipya la milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish”
Bw. Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hiyo mpya iliyoingia sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na uwezo wa friji hilo huku akiongeza kuwa Friji hilo pia litapatikana katika maduka mengine yote yanayouza vifaa vya kielektroniki jijini Dar.
“Katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani, watu wengi hutunza vyakula vyao kwenye mafriji na ni hulka ya wengi kuamka usiku kwa ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa na manufaa sana kwao kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia kutunza chakula katika hali ya usalama” alisema Kim.
Ofa hizi zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na Sabasaba, hii ni katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia bidhaa za LG zenye punguzo la bei
“LG Electronics daima inaendelea kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa zenye ubora na muonekana yakinifu ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa na toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya sokoni ni muendelezo wa matoleo yetu ya teknolojia ambayo yanatengenezwa na kuboreshwa kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja wetu” alisema Mr. Kim Taehoon
LG Electronics, Inc.
LG Electronics, Inc (KSE: 066570.KS) ni kampuni inayoogoza kimataifa kuleta teknolojia kwa matumizi ya umeme, mawasiliano ya simu na vifaa mbalimabli vya nyumbani. Tumeajiri takribani watu 87,000 kufanya kazi katika maeneo 113 duniani kote. Mnamo mwaka 2012 mauzo ya kimataifa yalifikia dola billioni 55.91 (KRW trillioni 59.04), LG inajumuisha vitengo vya biashara tano – vifaa vya burudani ya Nyumbani, Simu za Mawasiliano, Vifaa vya matumizi nyumbani, Viyoyozi vya majumbani & Nishati na kwenye Magari - na ni moja ya kampuni kiongozi wa kuzalisha TV Bapa, Vifaa vya simu, viyoyozi, mashine za kufulia nguo na friji. LG Electronicsni kampuni mwenzi wa 2013 ENERGY STAR ® .
Kwa habari zaidi kuhusu LG Electronics, tafadhali tembelea www.LGnewsroom.com.
No comments:
Post a Comment