Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 22 June 2015

RAIS WA INDIA NA WAZIRI MKUU WA INDIA WAMPOKEA RASMI RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU YA INDIA JUNI 19, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya Juni 19, 2015.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Majeshi ya India lililoandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika asubuhi ya Juni 19, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za kumkaribisha nchini India kwa ziara rasmi ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika Ikulu ya India mjini New Delhi, asubuhi ya Juni 19, 2015.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada katika kaburi la mpigania uhuru na muasisi wa taifa la India Mahatma Ghandi jijini New Delhi India Juni 19,2015.
Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment