Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 18 May 2015

TIGO YAZINDUA BIDHAA YA KIPEKEE YA UJASIRIAMALI KWENYE SIMU KWA WATEJA WAKE NCHINI TANZANIA


Tarehe 17, Mei 2015, Dar es Salaam – Tigo, kampuni yenye ubunifu zaidi wa kidijitali nchini na EduMe, inayotoa huduma ya kwanza ya kimataifa ya mambo ya elimu kupitia simu wamezindua bidhaa ya kipekee ya ujasiriamali kwenye simu kwa wateja wa Tigo nchini Tanzania.

Shule ya Biashara inawawezesha watumiaji kujifunza ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa bei nafuu kabisa kupitia kwenye simu yoyote ya mkononi. Tigo Tanzania, ambayo ni sehemu ya kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya simu na vyombo vya habari ya Millicom, ni ya kwanza barani Afrika kuzindua huduma kama hii.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha kidijitali Bw. Yaya N 'Djore alisema" Kampuni ya Tigo Tanzania ilituzwa ruzuku ya ubunifu kutoka GSMA Connected Women ili kutengeneza huduma ya "Shule ya Biashara” mafunzo ya ujasiriamali wa kwenye simu yanayolenga kuwaandaa wajasiriamali wenye kipato kidogo kuwa na ujuzi unaohitajika kuanza au kukuza biashara "

Somo linatumia hadithi za wamiliki wa biashara wa ndani na masomo yaliyochambuliwa ili kutoa mwongozo kwa watumiaji kupitia kila hatua muhimu ya kuanzisha na kuendesha biashara. Masomo yanaelezea mada kama vile, jinsi ya kuchagua wazo la kibiashara, jinsi ya kuongeza uelewa kuhusu biashara na jinsi ya kusimamia biashara yako. Masomo yanatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi au sauti kwa lugha ya Kiswahili na kufanya yapatikane kwenye simu yoyote, na kwa watu wenye uelewa mdogo wa lugha ya kiingereza na / au ngazi ya elimu. Baada ya kukamilisha masomo watumiaji wanaweza kupata vyeti vya ujasiriamali vya EduMe-Tigo. Pia watapata fursa ya kuomba mikopo midogo kupitia kwenye ushirikiano wa Tigo na Benki ya Afrika na Benki ya Wanawake ya Covenant (Tanzania) Ltd.

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Bw. Diego Gutierrez, alisema: "Tumefurahi kutoa huduma hii kubwa na mpya kwa wateja wetu. Kuna mahitaji makubwa ya elimu ya biashara nchini Tanzania kwa sababu wajasiriamali ndio wanaounda uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Kampuni ya Tigo ina dhamira ya kukuza maisha ya kidijitali na kubadilisha maisha. Elimu ni muhimu katika hili."

Mkurugenzi Mtendaji wa EduMe Bw. Jacob Waern, alielezea: "Tumefurahi kutoa fursa kwa mamilioni ya watu nchini Tanzania kupata mafanikio katika biashara zao. Dhamira yetu ni kuanzisha huduma mpya za simu zinazohusu elimu ambazo zitawawezesha wateja wetu kujifunza kwa wakati wowote na mahali popote.

Kutokana na kujikita kwao kwenye ubunifu katika masoko ya ndani na dhamira yao ya kutoa huduma tofauti kwa wateja, Kampuni ya Tigo ni mwenza sahihi wa EduMe."

Huduma ya Shule ya Biashara inapatikana kwa wateja wa Tigo. Wateja wanaweza kupata huduma hii kwa kupiga * 148 * 33 # au kwa kutuma ujumbe wenye neno Biashara kwenda 15633.

Ingawa huduma ilifunguliwa kwa watumiaji wachache mwezi Oktoba 2014, huduma mpya ambayo ni rahisi kwa watumiaji sasa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo. Hadi sasa, Shule ya Biashara ya Tigo imetoa zaidi ya masomo 100,000. Zaidi ya watumiaji 11,000 wameshatumia huduma hii, kati ya hao watumiaji 4,000 ni wanawake.

Kuhusu Tigo

Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania , ikijulikana kama “nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo mapya 500 yenye mtandao wa Tigo na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini. Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 7 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 100,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.

Tigo ni sehemu ya kampuni la Millicom, kampuni linaloongoza katika mawasiliano na vyombo vya habari, Kampuni lenye dhamira ya kukuza masoko barani Afrika na amerika ya Kusini. Kampuni ya Millicom huwa inaweka juhudi kubwa katika suala la kuleta huduma bunifu ya maisha ya kidijitare kwa wateja kwenye dunia inayochipukia katika masoko. Kampuni ya Millicom imeajiri zaidi ya wafanyakazi 16,000 na imetoa simu za mkononi, huduma ya setelaiti kwa wateja wake zaidi ya milioni 56. Ilianzishwa mwaka 1990, simu za Milicom za kimataifa zimetajwa kwenye NASDAQ OMX Stockholm chini ya nembo MIC.

“Tabasamu, Uko Pamoja na Tigo”

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz or wasiliana na:

John Wanyancha – Meneja Mawasiliano

Mobile: 0658 123 089

john.wanyancha@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment