Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 20 May 2015

RAIS WA MSUMBIJI ALIPOTEMBELEA CHUO CHA DIPLOMASIA

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR), Balozi Mwanaidi Maajar huku Mkuu wa Chuo hicho Balozi Mohammed Maundi akisikiliza wakati viongozi hao wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipotembelea Chuoni hapo tarehe 18 Mei, 2015 wakati akiendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini. Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini, Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Maundi alipotembelea Chuoni hapo wakati wa ziara yake hapa nchini. 
Balozi Maundi akiwatambulisha baadhi ya Wahadhiri wa Chuo hicho kwa Mhe. Rais Nyusi.


Juu na Chini: Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Wahadhiri, Wanafunzi na Wageni mbalimbali alipotembelea Chuo cha Diplomasia (CFR).
Wajumbe wakifurahia jambo wakati Rais Nyusi (hayupo pichani) alipozungumza nao.
Mhe. Rais Nyusi akifurahia zawadi ya picha ya kuchora inayowaonesha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel aliyozawadiwa alipotembelea Chuo cha Diplomasia. 
Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Msumbiji pamoja na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia (wa kwanza kushoto) ambaye ni Waziri anayeongozana nae kwenye ziara hii.

Mhe. Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
Rais Nyusi akiangalia bango linalosomeka "CHUO HIKI KILIKUWA CHUO CHA ELIMU YA JUU KWA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA" ikiwa ni jina la awali kabla Chuo cha Diplomasia hakijaanzishwa.
Mhe. Rais Nyusi akiangalia Jiwe la Msingi la kuanzishwa kwa Chuo hicho.

No comments:

Post a Comment