Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 22 May 2015

KITUO CHA KUZALISHA UMEME KWA NJIA YA GESI CHA KINYEREZI I KUKAMILIKA MWAKA HUU

Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango. Pichani ni Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg. Robert Masatu na Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano.
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi I.
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi I.
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi I kwa juu.
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi I kwa juu.
Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.

“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.

Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.

Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.

“Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.

Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.

No comments:

Post a Comment