Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 23 May 2015

BENKI YA NMB YAPELEKA HUDUMA YA CHAP CHAP MIKOANI

Benki ya NMB imepokelewa kwa nguvu na wananchi wa mikoa ya Arusha, Morogoro, Dodoma, Singida, Mtwara na Tabora na kampeni yake ya kuhamasisha watanzania wengi zaidi wasio na akaunti kufungua kupitia NMB bila usumbufu wa kuleta taarifa nyingi zaidi ya kitambulisho.

Huduma hiyo inayoitwa NMB Instant Account imekuwa kipenzi cha watanzania. Huduma hiyo inamuwezesha mtu yoyote anayetaka kufungua akaunti ya NMB kufanya hivyo kwa dakika 10 tu huku akiondoka na kadi ya ATM papo hapo. Pia mteja anaweza kufuatwa popote alipo na kufunguliwa akaunti hiyo kwa haraka huku akiendelea kupata huduma zingine za kibenki kama NMB mobile – kutuma na kutoa pesa kwa kutumia simu ya mkononi.

Fuatilia mikutano ya NMB kwenye maeneo yako leo – kwa mikoa ya Arusha, Morogoro, Tabora, Dodoma, Singida na Mtwara ujipatie akaunti ya NMB Chap Chap Instant Account.
Steven Ndaki Mkazi wa Homboro mkoani Dodoma akifungua akaunti ya Chap Chap Instant Account alipotembelea kwenye gari la kampeni la NMB.
Glory Mushi wa Homboro Dodoma akipata huduma za kufungua akaunti ya chap chap.
Ufunguaji wa akaunti za chap chap ukiendelea katika mji wa Homboro - Dodoma.


No comments:

Post a Comment