Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 7 March 2015

BENKI YA NMB KATIKA SHEREHE YA KUMKARIBISHA MKURUGENZI WAO MPYA

Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wao mpya, Ineke Bussemaker ambaye anachukua nafasi ya Mark Wiessing. Wiessing amepangiwa kituo kingine cha kazi ndani ya Benki ya Rabobank iliyopo Brazil.
Wiessing ataanza rasmi majukumu yake Brazil mwezi wa tano mwaka huu.

Ineke Bussemaker anakuja NMB akitokea Uholanzi ambako alikuwa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Malipo katika Benki ya Rabobank hivyo ni mtu mwenye uzoefu wa juu wa masuala ya kibenki na biashara ya kimtandao, utaalamu ambao utaisaidia benki ya NMB kukua zaidi.

Kabla ya RaboBank, Ineke alishika nyadhifa mbalimbali za juu katika benki za Citibank, ABN Amro ya Uholanzi, Uingereza na Denmark.

Mark Wiessing anaiacha NMB ikiwa imekua kwa kasi kwa miaka minne ya uongozi wake, ambapo NMB ina matawi zaidi ya170 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima, huku ikiwa na wateja zaidi ya milioni mbili.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa NMB, Ineke Bussemaker akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, uongozi wa juu wa benki na bodi ya wakurugenzi wa NMB katika hafla iliyoandaliwa na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi wa NMB, uongozi wa juu wa benki hiyo pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa NMB, Ineke Bussemaker akisalimiana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Juma Reli katika hafla iliyoandaliwa na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi wa NMB, uongozi wa juu wa benki hiyo pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa NMB, Ineke Bussemaker katika mazungumzo na Meya wa Ilala, Jery Slaa na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Prof Joseph Semboja katika hafla iliyoandaliwa na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa juu wa benki hiyo pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.




No comments:

Post a Comment