Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 25 February 2015

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA NA SHULE YA MSINGI MWANAKWEREKWE, ZANZIBAR

Benki ya NMB imetoa msaada wa zaidi ya madawati 50 kwa ajili ya kusaidia Shule ya Msingi ya Mwanakwerekwe na vitanda vya wagonjwa kwa ajili ya hospitali ya Mnazi Mmoja, misaada yote ikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 10.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas akikabidhi vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ali Abdalla kwaajili ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas alisema msaada huo ni mwitikio wa NMB kusaidiana na wananchi pamoja na serikali katika kutatua changamoto za elimu na afya nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ali Abdalla alipokea vifaa vya hospitali kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein na kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu na afya.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas akiwaelekeza jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanakwerekwe baada ya Benki ya NMB kukabidhi msaada wa madawati 50.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, akikabidhi madawati kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanakwerekwe.

Millardayo.com

No comments:

Post a Comment