Meneja
wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha bahati na sibu ya shindano la Tutoke na Serengeti,
linaloendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Bw. Hassan Mfaume ameibuka mshindi
katika Shindano hilo. Kulia ni Msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha,
Abdallah Hemedy na kushoto ni Auditor kutoka PricewaterhouseCoopers,
Golder Kamuzora. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es
Salaam.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha bahati na sibu ya shindano la “Tutoke na Serengeti” linalo endeshwa na kampuni hiyo, ambapo Hassan Mfaume ameibuka mshindi katika shindano hilo. Kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Abdallah Hemedy.
Akiongea baada ya droo iliyoshuhudiwa na waandishi wa habari pamoja
na Bwana Abdallah Hemedi mwakilishi wa bodi ya michezo ya bahati na sibu
Tanzania, Bwana Rugambo Rodney-Meneja Chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager alisema
Bwana Hassan ameshinda safari ya watu wawili iliyolipiwa gharama zote ikimaanisha
kwamba anaruhusiwa kwenda na mwenza wake na SBL watagharamia kila kitu kuanzia malazi,
usafiri pamoja na vivutio mbalimbali.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha bahati na sibu ya shindano la “Tutoke na Serengeti” linalo endeshwa na kampuni hiyo, ambapo Hassan Mfaume ameibuka mshindi katika shindano hilo. Kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Abdallah Hemedy.
Kampuni ya SBL leo imemzawadia Bwana Hassan Mfaume mkazi wa Mabibo ziara ya kwenda kutembelea hifadhi ya
taifa ya Serengeti iliyolipiwa na kampuni hiyo mara baada ya kuibuka mshindi wa
droo ya Tutoke na Serengeti iliyofanyika leo makao makuu ya SBL yaliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Akiongea kwa njia
ya simu Bwana Hassan ambaye alikua kikazi Mwanza alionekana kushangazwa na kushitushwa
baada ya kusikia taarifa kwamba amekuwa mshindi. Aliishukuru kampuni ya SBL kwa
kile alichokiita zawadi murua ya kipindi hiki cha sikukuu.
Hii imekuja wiki
moja tu baada ya Rukia Almasi, ambaye ni Mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda-Morogoro
kutuzwa ushindi wa Limo Bajaj katika kampeni hii inayoendelea.
Rodney aliwasihi watanzania waendelee kushiriki
kwani zawadi za kushindaniwa zipo nyingi. Aliongeza kwamba kampuni imelenga katika
kuinua utalii wa ndani ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha sehemu ya faida kwa wateja
wake baada ya mafanikio mazuri yaliyopatikana katika mwaka husika.
Kampeni ya Tutoke na Serengeti
wameungana na B-Pesa wataalam wa teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua
mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha
kwa washindi mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi.
Ili kushinda, unachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Serengeti
Premium Lager na angalia chini ya kizibo atakuta namba ambazo zinatakiwa kutumwa kwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenda namba 15317
ili kuingia katika droo.
Kwa taarifa
zaidi :-
Tembelea ukurasa wa Facebook wa Serengeti Premium Lager na
Twitter.
KUHUSU
SERENGETI BREWERIES LIMITED
Serengeti Breweries Limited ni kampuni ya bia ambayo huandaa,
kuzalisha na kuuza vinywaji vilivyotengezwa na shairi, ngano na mtama nchini
Tanzania.
Ikiwa na makao yakemakuu jijini Dar es Salaam, SBL hutengeneza vinywaji
vifuatavyo:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker
Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and
Guinness®.
SBL piahusambazavinywajimbalimbalivikalizakimataifakama Smirnoff
Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and
Gilbeys Gin®.
Serengeti Breweries Limitednikampunimwenzaya East African
Breweries Limited/ DIAGEO PLC
No comments:
Post a Comment