Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 5 November 2014

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA PROMOSHENI IJULIKANAYO KAMA "CHINI YA KIZIBO" (TUTOKE NA SERENGETI)

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya Uzinduzi wa shindano lijulikanalo kama, Chini ya kizibo (tutoke na Serengeti), ikishirikiana na B Pesa, ambampo washindi watapelekwa Mbuga za wanyama, katikati ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface na kushoto ni Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya B Pesa, shekilango jijini Dar es Salaam. 

Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface, akiwaelezea waandishi wa Habari (hawapo Pichani), namna kampuni hiyo inavyoshiriki katika shindano la Chini ya Kizibo (Tutoke na Serengeti) wakati wa mkutano na waandishi uliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Shekilango jijini Dar es Salaam. 

Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo (kushoto) akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna kampuni ya Bia ya Serengeti ilivyojiaandaa kikamalifu na zawadi kibao na Shindano lijulikanalo kama, Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti)

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa shindano lijulikanalo kama, Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti), ikishirikiana na B Pesa, ambampo washindi watapelekwa Mbuga za wanyama. Katikati ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface na kushoto ni Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya B Pesa, shekilango jijini Dar es Salaam. 

Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface, (katikati) na Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, (Kulia) wakishikana mikono kama ishara ya kuungana pamoja katika kampeni ijulikanayo kama , Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti). Hafla hiyo ilifanyika ndani ya  ofisi za B Pesa  shekilango jijini Dar es Salaam. 
Bw. Salil Abbas, Marketing Manager wa B-Pesa akiteta jambo na Bw. Ephraim Mafuru ambaye ni Marketing Director wa SBL wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.


Bajaj zinazoshindaniwa katika shindano la Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti) 

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, akiendesha moja ya Bajaj ambazo zitashindaniwa katika shindano lijulikanalo kama Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti), wa pili nyuma ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface.

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, akiendesha moja ya Bajaj ambazo zitashindaniwa katika shindano lijulikanalo kama Chini ya kizibo (Tutoke na Serengeti), wa pili nyuma ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface.

KAMPUNI ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager imezindua mpango kabambe unaoitwa Tutoke na Serengeti wa kuwazawadia wateja wake kwa kuwapa fursa ya kufaidi utalii wa ndani kwa kuwapeleka kwenye mbuga za wanyama tunapoeleka mwanzoni mwa shamrashamra za sikukuu za mwisho wa mwaka. Promosheni hiyo inalenga kuwafikia wateja wapatao milioni 20 ambao watapata fursa ya kujishindia fedha taslimu na zawadi nyingine nyingi.

Kuhakikisha kwamba kampeni hiyo inafanikiwa, Serengeti imeshirikiana na B-Pesa, wataalamu wa teknolojia ambao hivi karibuni walizindua huduma mpya ya kutuma pesa ambao watakuwa na jukumu la kuwatumia washindi pesa popote nchini. Washindi katika kampeni hii wana fursa ya kushinda zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 100 ambazo zimegawanywa katika mafungu ya shilingi 5,000. Wateja pia watapata nafasi ya kushinda  bia za bure watakaponunua Serengeti premium Lager na kufunua chini ya kizibo pamoja na punguzo la bei ya bia ya shillingi 300 kwenye baa yoyote Tanzania.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za B-Pesa zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam, Meneja wa masoko wa   bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo pia alizungumzia zawadi zitakazotolewa kwa washindi. “Tutatoa zawadi za Bajaj sita aina ya Limo zijulikanazo kama Serengeti Bajaj ambazo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 7,’’ alisema.

Pia SBL itatoa nafasi kwa wenza sita katika msimu huu wa sikukuu kutembelea mbuga za wanyama. Kampeni hii kwa mujibu wa Allan Chonjo itafanyika mwaka mzima na inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miezi 3. Wateja watatakiwa kununua bia ya Serengeti na kuangalia ndani ya kizibo ili kujionea kama wameshinda zawadi hizo. Alisisitiza kuwa shindano hili halitaongeza bei ya bia.

Naye Mkurugenzi wa Serengeti Breweries bwana Ephraim Mafuru ambaye pia alihudhuria katika mkutano wa wanahabari alisema kuwa promosheni hiyo ina lengo la kuwazawadia wateja wao na kwamba ni njia pekee ya kuwatambua wateja wao.

Kwa upande wake Meneja wa masoko wa B-Pesa Bwana Sallil Sadak, alisema: “Tunayo furaha sana kushirikiana na Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kampeni hii  kupitia huduma zetu na tuna uhakika kuwa promosheni hii itafanikiwa kwa kiwango kikubwa

KUHUSU KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI
Kampuni ya Bia ya Serengeti inahusika na upishi, matengenezo, masoko na mauzo ya vileo vinavyotokana na ngano, shayiri, mihopi na mtama nchini Tanzania.

Ikiwa na makao yake makuu jinini Dar es Salaam, bidhaa za Kampuni ya Bia ya Serengeti ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®

Kampuni hiyo pia ni msambazaji pekee wa vinywaji vikali vinavyofahamika kimataifa ikiwa ni pamoja na Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.

Kampuni ya Bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya East African Breweries Limited/ DIAGEO PLC

No comments:

Post a Comment