Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 2 October 2014

SULUHISHO LA AJIRA KWA VIJANA NCHINI LAPATIWA TIBA

Mkurugenzi wa TSGC, Bw. Victor Tesha.

Mkurugenzi wa TSGC, Bw. Victor Tesha akiwasilisha mada kwa vijana Mkoani Arusha.

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini linaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa ujio wa mikopo yenye riba nafuu nchini. Mikopo hiyo ambayo itaanza kutolewa rasmi kwa awamu ya kwanza mwezi wa 12 mwaka huu itakuwa na masharti nafuu sana ikilinganishwa na aina nyingine za mikopo ambayo ilishawahi kutolewa nchini.

Akizungumza hayo mjini Arusha, Mkurugenzi wa Tanzania SME Growth Centre (TSGC), Bw. Victor Tesha, alibainisha baadhi ya sifa hizo kuwa ni:-

1. Riba kwa mikopo hiyo itakuwa ni asilimia 5 tu.
2. Wakopaji watakopeshwa vifaa vya uzalishaji tofauti na mikopo mingine ambayo hupewa fadha cash.


Aidha hii itakuwa ni fursa nyingine kwa vijana wajasiriamali kuimarisha mitaji yao kwa aina hii ya mkopo kwa kubuni miradi na kupatiwa vifaa kwa ajili ya miradi yao. Bw.Tesha pia alifafanua kuwa pamoja na kupatiwa mikopo hiyo kutakuwepo na 'close monitoring' ya miradi yenyewe ikiwa ni pamoja na vijana hao kupatiwa ushauri elekezi ya namna ya kuimarisha miradi yao ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Masharti mengine ya mkopo huu ni kwa vijana ambao hawana mradi wowote ambao upo tayari kwa ajili ya kuuendeleza wanaweza kupata mkopo huo endapo tu wataunda vikundi vya watu kumi vinavyotambuliwa kisheria na kupatiwa vifaa vya kuanzisha mradi walioukusudiwa.

Kama vijana watatumia fursa hii vizuri tatizo la ukosefu wa ajira unaweza kupunguzwa na vijana wakajenga uwezo kiuchumi nchini. Vijana Itumieni fursa hii.

Bw. Tesha alisisitiza kuwa mikopo hio ikianza itaisadia uchumi wa nchi ku kuwa kwa vile utatengeneza wazalishaji wengi kuliko uchumi ulivyo hivi sasa wa kununua na kuuza ambao hautengenezi ajira nyingi kwa vijana. 

No comments:

Post a Comment