Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 6 October 2014

MENEJIMENTI YA NBC YAKUTANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU LEO

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Mizinga Melu  (wa tatu kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa Mizinga Melu alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.

Rais Jakaya Kikwete akishikana mikono na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) wakati  Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Mizinga Melu (wa pili kushoto) alipokwenda Ikulu, Dar es Salaam kumuaga mheshimiwa rais. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muda, Pius Tibazarwa na Meneja Mahusiano, William Kallaghe (kulia).

Rais Jakaya Kikwete akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa  NBC, Pius Tibazarwa (wa pili kulia) mara baada ya hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa, Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Mizinga Melu na  Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Mizinga Melu (wa pili kushoto), alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Pius Tibazarwa na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment