Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 28 September 2014

WAFANYAKAZI WA NBC WAADHIMISHA SIKU YA MOYO DUNIANI KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA VIJANA NA WATOTO WANAOSUMBULIWA NA MAGOMJWA YA MOYO.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakianza matembezi ya hisani ya takribani Kilomita 10 jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni moja ya matukio ya benki hiyo kudhimisha Siku ya Moyo Duniani ambapo kiasi cha pesa watakachochangisha kitapelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo. Siku ya Moyo Duniani huadhimishwa kimataifa Septemba 29 kila mwaka.

Hapa baadhi ya wafanyakazi hao wakipita katika barabara ya Ocean Road kulekea maeoneo ya Coco Beach wakitokea makao makuu ya beni hiyo katika Tawi la Corporate, Posta Mpya.

Hapa ni daraja la Salender, kwa moyo wa kujitolea wafanyakazi hawa wa NBC wakiendelea na matembezi hayo ili kupata fedha kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Safari inaendelea, hapa baadhi ya wafanyakazi hao wakikaribia kufika mwisho wa matembezi yao hapa ikiwa ni Barabara ya Kenyatta wakielekea Coco Beach.

Hapa wakiwa katika shangwe baada ya kumaliza matembezi hayo kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi maeneo ya Coco Beach kama umbali wa kilomita 10.

Baada ya kumaliza matembezi hayo wafanyakazi hao wakipiga picha ya pamoja kuonyesha ushindi na mshikamano wao katika kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na matatizo ya magonjwa ya moyo.

No comments:

Post a Comment