Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 5 September 2014

AZANIA BENKI WAZINDUA AKAUNTI MPYA YA DHAMIRA

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira (Dhamira Account) uliofanyika jana kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo, Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Singili.

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Singili. 

Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Singili akimuelekeza namna ya kujaza fomu, Bi. Naomi Mapunda ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akauni hiyo ya Dhamira.

Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Azania.

Mkurugenzi mtendaji wa Azania benki, Charles Singili amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadae.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira, Singili alisema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapunguza tatizo la umasikini kwa wananchi.
 
Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakipatiwa elimu kuhusu faida za kutunza fedha zao, itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.
 
“Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua akaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote” alisema Singili.
 
Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.
 
Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 na kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.
 
“Dhamira akaunti itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12,” alisema.

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment