Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 15 June 2014

WAFANYAKAZI WA CITI BANK TANZANIA WATOA MSAADA KWENYE KITENGO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI, TANDIKA JIJINI DAR

Wafanyakazi wa Citi Bank Tanzania wameweza kujichangisha wenyewe kwa wenyewe na kupata fedha zilizofanikisha ukarabati wa jengo litakalotumika kama jiko la kupikia na ukumbi wa kulia chakula kwenye kitengo cha watoto wenye ulemavu wa akili cha shule ya msingi ya Tandika, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hao wameamua kufanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kusaidia watu wenye mahitaji. Mbali na ukarabati huo, waliweza pia kujitolea kufanya usafi wa mazingira ya eneo la shule hiyo.


Baadhi ya ya wafanyakazi wa Citi Bank wakiwa wamejumuika pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Tandika ambao wana ulemavu wa akili.


Wanafunzi hao wakifurahia ugeni huo uliowatembelea


Meneja Mkuu wa Citi Bank Tanzania, Noel Sangiwa (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili, Tandika, Mary Batamula (katikati) wakishirikiana kukata utepe kuashiri uzinduzi rasmi wa jengo litakalotumika kama jiko la kupikia na ukumbi wa kulia chakula.


Wafanyakazi wa Citi Bank wakifanya usafi wa mazingira katika eneo la shule ya msingi, Tandika, ambako kuna kitengo cha watoto wenye ulemavu wa akili.

Bofya hapa kwa picha zaidi.

No comments:

Post a Comment