Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 13 October 2025

VODACOM YATOA TUZO KWA WAFAKAZI KATIKA HITIMISHO LA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi wa Sheria wa Vodacom Tanzania Plc, Olaf Mumburi (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mfanyakazi Francis Baragwiha (katikati) wakati wa hafla ya “Usiku wa Mabingwa” iliyosherehekea wafanyakazi waliochangia mafanikio ya kampuni hiyo katika kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidijitali, Belinda Wera. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

“USIKU WA MABINGWA” WAADHIMISHA UBORA, SHAUKU NA MIAKA 25 YA HUDUMA

DAR ES SALAAM, TANZANIA – OKTOBA 10, 2025: Vodacom Tanzania PLC imehitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa hafla ya utoaji wa tuzo iliyopewa jina la “Usiku wa Mabingwa”. Hafla hiyo iliwaenzi wafanyakazi wanaohudumia wateja pamoja na timu za usaidizi ambao, kwa kujitolea kwao bila kuyumba, wameendelea kuandika historia ya Vodacom katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa VodacomMkurugenzi wa Rasilimali Watu, Vivienne Penessis, aliwasifu wafanyakazi wa usaidizi kama mhimili wa mafanikio ya chapa ya Vodacom.

“Usiku wa leo tumekusanyika kuwaenzi mashujaa wa safari yetu ya huduma kwa wateja. Uaminifu wenu, shauku yenu na uvumilivu wenu ndio sababu Vodacom inaendelea kuongoza katika ubora wa huduma,” alisema Penessis.

 

Akielezea safari ya miaka 25 ya kampuni, Penessis aliongeza kuwa mafanikio ya Vodacom hayapo tu katika teknolojia, bali pia katika uhusiano wa kibinadamu uliodumu kwa muda mrefu.

“Urithi wa Vodacom haupo tu katika teknolojia, bali uko katika mahusiano ya kibinadamu tuliyojenga kwa muda. Watu tunaowaenzi leo wamekuwa sehemu muhimu ya ukuaji wetu — si kwa idadi tu, bali kwa uaminifu, sifa na matokeo chanya,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Belinda WeraMkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidijitali, alibainisha kuwa hafla hiyo inalenga kutambua juhudi za timu zinazowahudumia wateja moja kwa moja pamoja na wale wanaofanya kazi nyuma ya pazia.

“Tuzo zilizotolewa usiku huu ni zaidi ya utambuzi. Ni taswira ya utamaduni wa Vodacom, kama unavyoonyeshwa na watoa huduma wetu katika maeneo yote ya huduma kama vile kituo cha huduma kwa wateja (Call Centre), ofisi za ndani (Back Office), maduka ya huduma, pamoja na timu za usaidizi wa mtandao na TEHAMA,” alisema Wera.

“Usiku wa Mabingwa” uliwaenzi wafanyakazi wa Vodacom wanaoishi kwa vitendo nguzo kuu za kampuni hiyo — wale wanaounganisha timu kufanikisha matokeo, wanaobuni kwa ujasiri kwa ajili ya kesho, wanaojifunza haraka kupitia majaribio, na wanaojenga uaminifu wa wateja kwa kutoa huduma bora.

Hafla hiyo pia ilipambwa na vipaji vya ubunifu kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom, waliotoa burudani kupitia muziki, vichekesho, ushairi na uchezaji, huku watangazaji wa hafla (MCs) wakionyesha ubunifu na utofauti unaoendana na ubora wa huduma kwa wateja.

Katika hafla hiyo, jumla ya tuzo 38 zilitolewa kutambua michango ya kipekee kutoka kwa timu na idara mbalimbali — ikijumuisha tuzo 37 za mtu binafsi na tuzo moja ya timu iliyojitokeza kwa utendaji wa kipekee.




No comments:

Post a Comment