 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) (katikati) akiwaongoza wadau wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi (wa pili kushoto) kuzindua Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini yanayoratibiwa na Benki ya NBC kwa ushirikiano na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Hafla ya uzinduzi huo huo imefanyika Makao Makuu ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (kushoto), Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Gift Kyando (wa pili kulia) na Mratibu wa Uandishi wa Insha kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia, Lazaro Mnkeni (kulia) pamoja na wawakilishi wa wanafunzi kutoka shule za Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kushoto) (wa pili kushoto) wakibadilishana miongozo ya Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini yanayoratibiwa na Benki ya NBC kwa ushirikiano na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). |
 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) (kulia) akipokea risala maalum kuhusu Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini yanayoratibiwa na Benki ya NBC kwa ushirikiano na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoka kwa mwanafunzi Daniel Mwandolela, muhitimu wa kidato cha nne kutoka Sekondari ya Wanaume ya Feza ya jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini. |
 |
Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi (wa tatu kulia) akifafanua mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) (kushoto) kuhusu Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini. |
 |
Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mashindano ya Uandishi wa Insha na Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi wa Sekondari nchini. |
- Zawadi ya Shilingi Milioni 10 Kutolewa kwa Mshindi wa Jumla
Dar es Salaam, Mei 25, 2025 – Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb), amezindua rasmi mashindano ya kitaifa ya NBC Essay Challenge na NBC Business Idea Competition, yenye lengo la kuibua vipaji na kukuza ubunifu miongoni mwa wanafunzi wa sekondari nchini.

Mashindano haya, yanayoratibiwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI, yanatarajiwa kuwafikia zaidi ya wanafunzi milioni moja wa shule za sekondari za umma na binafsi kote nchini. Lengo kuu ni kuchochea ubunifu, ujasiriamali, nidhamu ya fedha na usimamizi bora wa rasilimali miongoni mwa vijana.
“Mashindano haya ni fursa kwa watoto wetu kupima na kuthibitisha ubora wa mawazo yao, hasa kwenye masuala ya kiuchumi. Nataka taarifa hizi ziwafikie wanafunzi wote nchini,” alisema Prof. Mkenda.
Mshindi wa jumla wa mashindano haya atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Shilingi Milioni 10, huku wengine wakipata zawadi kama vile kompyuta mpakato, simu, vitabu, mabegi na vifaa vya kujifunzia.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, alisema mashindano hayo yanalenga kujenga kizazi chenye uelewa wa kina kuhusu fedha, akiba na ushindani wa kibiashara. Alisema ni sehemu ya suluhisho kwa changamoto ya elimu duni ya kifedha miongoni mwa vijana, ikizingatiwa kuwa asilimia 35 tu ya vijana chini ya miaka 25 wana akaunti ya benki, kulingana na utafiti wa FINSCOPE 2023.
“NBC tupo hapa kutatua changamoto hii kwa kuwafikia vijana kuanzia shule za sekondari kupitia mashindano haya ya kiubunifu,” alisema Bw. Sabi.
Wanafunzi 200 bora watapata fursa ya kujiunga na NBC Student Mentorship Club, mpango maalum wa kuwawezesha kupata mafunzo ya fedha na ujasiriamali wakati wa likizo.

Kwa upande wa ushiriki, akaunti ya benki ya NBC ni sharti muhimu, kwani zawadi zote za kifedha zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wanafunzi – kupitia huduma za NBC Student Account na Chanua Account.

Wanafunzi na walimu waliohudhuria walieleza kufurahishwa na fursa hiyo, wakisema itasaidia wanafunzi kujifunza nidhamu ya kifedha na kujiandaa vyema kwa ushindani wa ajira na biashara.
No comments:
Post a Comment