Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Tuesday, 18 March 2025

YAS TANZANIA YAANDAA FUTARI MAALUMU KWA WATEJA WAKE ZANZIBAR


Zanzibar, 14 Machi 2025 – Yas Tanzania imefanya hafla maalumu ya futari na wateja wake wa Zanzibar katika Hotel Verde, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 100 tangu mabadiliko rasmi ya chapa kutoka Tigo, TigoZantel na Tigo Pesa kwenda Yas na Mixx by Yas.



Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa, washirika wa kibiashara, wateja wa Yas & Mixx by Yas, na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa aliipongeza Yas Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa Zanzibar kupitia huduma za mawasiliano pamoja na huduma za kifedha kwa njia ya simu. Vilevile alitumia fursa hiyo kuishauri Kampuni ya Yas Tanzania kutuma jumbe za kuhamasisha amani kwa wateja wake kwakua mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi.


"Yas Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kuwahudumia wateja wake na jamii ya Zanzibar kwa ujumla. Hata hivyo, kwa kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, naomba kampuni hii itumie majukwaa yake mbalimbali kuhamasisha amani, utulivu, na mshikamano miongoni mwa wananchi," alisema Mhe. Kitwana.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Fedha wa Yas Tanzania, Ndugu Innocent Rwetabura, aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wake katika kufanikisha mabadiliko ya chapa za Yas na Mixx by Yas, ambayo yameleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya mawasiliano nchini.

"Tunaposherehekea siku 100 za Yas na Mixx by Yas, tunajivunia kuwa tumeweza kuwa karibu zaidi na wateja wetu na kuwafungulia fursa nyingi za kidijitali. Katika kipindi hiki kifupi, tumepokea mapokezi chanya kutoka kwa wateja wetu, na tumeendelea kuwekeza katika teknolojia na huduma bora ili kuimarisha zaidi uzoefu wao," alisema Rwetabura.

Katika hotuba yake, Rwetabura alieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika siku 100 za Yas na Mixx by Yas, ikiwa ni pamoja na:
  • Tuzo mbalimbali za umahiri: Yas imepokea tuzo za kimataifa na kitaifa, ikiwemo kutoka kwa Ookla na TEHAMA Awards, pamoja na kutambuliwa na TRA kama mlipaji mkubwa wa kodi katika Ushuru wa Forodha.
  • Ushirikiano wa kimkakati: Yas imeanzisha ubia na taasisi mbalimbali kama Zanzibar Petroleum Limited (ZPL), DSE, na e-Government Agency Zanzibar (EGAZ) ili kuimarisha huduma zake kwa Watanzania.
  • Uwekezaji katika miundombinu: Kampuni imeongeza idadi ya minara yake nchini hadi kufikia zaidi ya 4,000 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na intaneti yenye kasi.
  • Kampeni ya "Magift ya Kugift": Kupitia promosheni hii, zaidi ya Watanzania 1,300 wamenufaika kwa kupata zawadi zikiwemo magari mawili mapya, zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 840, na simu janja zaidi ya 540.
Rwetabura aliwashukuru wateja wa Zanzibar kwa kuendelea kuunga mkono Yas na Mixx by Yas, akisisitiza kuwa kampuni itaendelea kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja wake.

"Zanzibar ni sehemu muhimu ya safari yetu ya kuwafungulia Watanzania fursa za kidijitali. Tunajivunia wateja waaminifu ambao wameendelea kuwa nasi katika mabadiliko haya makubwa. Ahadi yetu ni kuendelea kuboresha huduma zetu ili ziwe za viwango vya kimataifa," aliongeza.

Katika hitimisho la hafla hiyo, Yas Tanzania iliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uchumi wa visiwa hivyo kupitia huduma zake za kidijitali na mawasiliano.

Kuhusu Yas na Mixx by Yas Tanzania

Yas Tanzania (iliyojulikana hapo awali kama Tigo Tanzania) ni Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwenye utoaji huduma za kidigitali na mawasiliano nchini Tanzania. Ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitatu. Mixx by Yas (iliyojulikana hapo awali kama Tigo Pesa) imekuwa kinara kwenye utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu ikihudumia zaidi ya wateja milioni 23 kote nchini. Kama sehemu ya Axian Group—kinara wa mawasiliano barani Afrika—Yas Tanzania inatoa huduma za kidijitali zisizo na kifani kupitia mtandao wake mpana, ikiwa ni pamoja na upatikanaji mkubwa wa 4G na kasi ya juu ya 5G. Yas inaendelea kuwaunganisha Watanzania popote walipo, ikichochea mustakabali wa kidijitali Tanzania. Huduma zetu za kifedha kwa njia ya simu, sasa zikifahamika kama Mixx by Yas, zinawawezesha watumiaji kupata huduma za kifedha zilizo salama, rahisi na nafuu, zikiwa zimebuniwa kusaidia jamii kustawi katika ulimwengu wa kidijitali unaokua kwa kasi. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea www.yas.co.tz au wasiliana na:

Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano wa Kampuni
Barua pepe: woinde.shisael@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment